Nena Mungu sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA
1. Nena rohoni Yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, “Huachwi upweke.”
Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.
Kila siku unene, Vile kwa upole.
Nong’oneza [kwa pole] wa upendo:
“Daima utashinda, Uhuru ni wako.”
Nisikie maneno: “Huachwi upweke.”
2. Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa, Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi.
3. Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yako tena, Daima kusifu.
Cherubim Singers, Nairobi South SDA.
F. Campana as Writer, Adapted by Leander Lycurgus.
From Nyimbo Za kristo 013