Siku Moja/Watoto Walia Lyrics sung by The Gospel Train
Siku Moja/Watoto Walia Lyrics sung by The Gospel Train
1. Siku moja niliondoka kutembelea rafiki yangu
Rafiki yangu kaniuliza "Umekuja kunicheka?
Kwamba mimi masikini, Mama mjane tena fukara
Mimi sioni haja tena ya ushirika,
Mungu amenitenga mbona nimuabudu?"
Refrain
Watoto walia, "Mama ako wapi, baba?"
Wajane wanauliza, "Yesu tumefanya nini?"
"Mbona tupitie haya? Mbona tusumbuke hivi?
Na sala sisi twatoa?"
2. "Mungu huyu mnayemwabudu, Ni Mungu wa aina gani?
Ni Mungu yule anayenyamaza tunapodhoofika,
Miaka mingi tumemwabudu, Kwa hali hata na mali
Jamani nielezeni sababu ya ushirika?
Mungu amenitenga mbona nimuabudu?"
Outro
Yesu anajibu "Mimi Baba ya mayatimu wote
Bwana, wa wajane wote, msiogope."
"Nitawalinda nitawachunga Mimi Mungu mwaminifu
Nilivyolinda mababu zenu Isaka kina Yakobo."
The Gospel Train, Kenya.
Heb 13:5 I will never leave thee, nor forsake thee.
Ps 34:18 The Lord is near to the broken hearted, and saves the CRUSHED in spirit.[bold is mine]
Zaburi 34:18 Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo; huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.
Comments
Post a Comment