Nashangaa - Kina Cha Pendo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Nashangaa - Kina Cha Pendo Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Nashangaa nashangaa, Kina cha upendo wa Mungu wanizunguka
Nashangaa tena nashangaa, Alivyo mwema kwangu siku zote
Kwa mapana marefu ya pendo, Nauona waziwazi
Pande zote amenizunguka, Naburudika kwenye pendo lako
Natembea bila wasiwasi, Katika pendo la Yesu
Refrain
Kina cha pendo la Yesu, Chazidi kina cha bahari
Hangaiko la machozi, Kwa Yesu ni furaha
Subiri ngoja uone Yesu, Atatenda kwa wakati
Kina cha upendo wa Yesu, Ni pendo lisilo kipimo
2. Nashangaa nashangaa, Maajabu ya pendo lake yanishangaza
Wema wake unadumu kwangu,Pendo lake linazidi kipimo
Nimeona marafiki wengi, Sijaona kama Yesu
Marafiki wa dunia hii, Wamejawa na pendo la herosi
Yesu ndiye rafiki wa kweli, Pendo lake linadumu.
Kurasini SDA Choir.