Tunataka Kumuona Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Tunataka Kumuona Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

1. 'Tunataka kumuona Yesu, Yesu
Eh, Bwana tunataka kumuona Yesu
Sisi tunataka kumwona Yesu,'
Walikuwa wayunani
Miongoni mwa waliopanda kwenda kuabudu
Walimwendea Filipo wakisema;

Refrain
'Bwana, Eh Bwana tunataka kumwona Yesu,
Tumesikia habari zake, Tunataka kumuona Yesu, Ooh,
Bwana, Eh Bwana tunataka kumuona Yesu,'
Walimwomba Filipo naye akawasikia

2. Mara ngapi wewe umeomba kumwona Yesu
Ili aseme na wewe, Akupe chakula cha mbingu
Waweka moyo wako mbali
Wafunga milango ya moyo
Fungua leo, uwe kama wale (kama wale) wayunani wa kale
Waliamua kumwomba Filipo kwa moyo

Outro
Bwana Yesu kafungua milango ya mbingu
Ameinyosha mikono yake
Angoja uitike ukichukua hatua kumuita
Mwite leo akungoja...
Atakusikiliza...

Kurasini SDA Choir.

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Damu Yake Lyrics sung by The Golden Gate Choir

Nyosha Mkono Wako Lyrics sung by Nyandema SDA Choir