Faraja Iko Wapi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Faraja iko wapi, Kati ya wanadamu?
Na wote wenye mwili ni dhaifu
Watafuta shauri Kati ya wanadamu
Walio kwenye shida na maovu
Refrain
Tafuta amani na watu wote, Uwe mtulivu,
Mpendeze Mungu (Mpendeze Mungu)
Fungu jema lakungojea, Umalizapo mwendo
Wa’ heri wenye moyo safi, Watamuona Mungu
2. Bwana ninakuomba, Shika kauli zangu
Ziwe zenye baraka kwa wengine
Waliobondwa mioyo warejeshe nguvu
Wasije kupotea, Wape nguvu.
Note
Kati ya wanadamu?; Katika
Wa’ heri = Wana heri
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 33, Bedi Score, Bedi Lyrics