Thursday, 30 April 2026

Ulipo Amini Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Ulipo Amini Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1-1

Ulipo amini na kuacha dhambi,

Ulipomrudia Bwana Mungu wako

Je ulikumbuka kumtumaini Mungu (Atawale shida)

Au ulipoanguka, Je uliomba msaada?


1-2

Ulipojutia machungu ya dhambi,

Na kutafakari ulivyolemewa mawazoni mwako

Umekosa faraja (Leo ndugu yangu)

Ukimtegemea utafarijika sana.


Refrain

(Oh Tazama) Tazameni watu wanavyoangamia

Wakifikiri kuna faida kupata vyote vya ulimwenguni

Mwishoni Maisha yao yanatoweka bila matumaini

Siku zote mwamini Yesu atakupigania


(Oh Tazama) Tazameni watu wanavyoangamia

Wakifikiri kuna faida kupata vyote vya ulimwenguni

Mwishoni Maisha yao yanatoweka bila matumaini

Siku zote mwamini Yesu atakupigania


2

Kila utendayo hata uwazayo yote ubatili

Bila roho wake utaenda wapi, Ufiche uso wako?

Bado anangojea (Bado anangojea) utafakari moyoni


Nafasi ni sasa umrudie Mungu vyote vya dunia

Utavisahau kwa neno la Mungu utaka salama

(Japo u dhaifu) Japo mwili dhaifu neno lake linatosha.


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 33, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...