Kando Ya Mto Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Kando ya mto ndipo tulipoketi
Tukikumbuka nyumbani Yerusalemi
Tukasikia amri ikitolea kwetu
Tuimbe wimbo wa Bwana nchi ya ugenini.
Refrain
Tungewezaje kuimba wimbo wa Bwana huko?
Tukatetea imani huko ugenini
Na leo wanatafutwa watakaotetea,
Imani ulimwenguni wakimkiri Bwana.
2. Kama mitume wengi walisimama
Wakitetea imani hata mauti
Kwa kusema waziwazi heri kufa na Yesu
Kuliko raha kitambo, Wewe wasemaje?
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 25, Bedi Score, Bedi Lyrics