Njooni Munywe Maji Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Njooni munywe maji ya uzima
Yapo bure kwa ajili yenu
Wenye kiu njooni munywe maji
Njooni nyote (Njooni nyote)
Refrain
Ukiyanywa yanatolewa bure
Siku zote hutaona kiu
Na ukioga utakuwa msafi,
Utabaki kuwa msafi (Na)
Chemichemi ya maji ya uzima
Njooni nyote munywe maji bure
Harakisha bado yapatikana
Katika kisima cha Bwana (Njooni nyote)
2. Kwenye kisima kuna msamaha
Unaotolewa na Yesu
Njooni nyote mnaosumbuka
Mkapumzike (Njooni nyote).
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 33, Bedi Score, Bedi Lyrics