Fungua Macho Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Mambo yanayotokea duniani sasa
Yote yanatimiza unabii,
Ulione na kuhusu nyakati za mwisho
Uamuzi wa mwisho ni juu yako
Kuokoa nafsi au kuiangamiza.
Refrain
Uasi umezidi usoni mwa nchi,
Na Mungu hawezi kuvumilia
Ni kama nyakati zile za Nuhu,
Watu walikula, wakinywa na kuoana
Sauti hii ni onyo kwa dunia,
Mungu amekusudia kuiangamiza.
2. Kila ukitega masikio,
Ni vita, ni maradhi, ni mambo ya kutisha
Yote yanatimiza unabii,
Ulione na kuhusu nyakati za mwisho
Uamuzi wa mwisho ni juu yako,
Kuokoa nafsi au kuiangamiza.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 30, Bedi Score, Bedi Lyrics