Mambo Ya Kesho Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Mambo ya kesho siyatambui
Nayapapasa ni giza kwangu
Yote ni mapenzi yake Muumba
Mambo ya kesho (ni) giza kwangu.
Refrain
Yote ni mapenzi yake Muumba
Siri zangu zote Bwana ajua
Nifiche nini Alfa Omega?
Mambo ya kesho (ni) giza kwangu.
2. Mambo ya kesho siyatambui
Kuna uzima mauti kwangu
Bwana niwezeshe kuyakabili
Niwe tayari (na) niwe wako.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 24, Bedi Score, Bedi Lyrics