Namshukuru Bwana Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Namshukuru Bwana kwa kila jambo
Namshukuru hata kwa majaribu
Yote ni mapenzi yake namshukuru,
Kila jambo na wakati wake,
Yote mapenzi yake.
Refrain
Kwenye moyo wangu fanya kituo Bwana
Kifuani mwako nitajiegemeza
Hofu na mashaka yote utanikingia Bwana
Namshukuru, Oh namshukuru,
Namshukuru, Oh namshukuru,
Kwa yote.
2. Namshukuru hata kwa milima mabonde,
Namshukuru kwa wakati wa hari
Hata kwa kimbunga nitamshukuru,
Kuishi kwangu ni Kristo pekee,
Na kufa ni faida.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 24, Bedi Score, Bedi Lyrics