Mbinguni Kulikuwa Kimya (Dhambi Zangu) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Mbinguni kulikuwa kimya,
Shujaa akashuka chini
Kabeba dhambi za dunia msalabani
Walo wake wakamkataa
Akabeba, dhambi zao
Refrain
Dhambi zangu, Akachukua msalaba
Dhambi zangu, Bwana akasulubishwa
Kashika njia, Kuelekea Kalvari
Dhambi zangu
2. Leo hii Bwana atuita,
Aita kwa upole mwingi
Njooni sasa mpo huru njooni kwangu
Msiifanye migumu mioyo
Njooni wote, Muwe huru.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 24, Bedi Score, Bedi Lyrics