Tulipokuwa Wenye Dhambi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Tulipokuwa wenye dhambi, tulipotea mbali
Kama wana wa Mungu tusilale, Tusijetenganishwa na Mungu
Sote kama wahitaji, dhambi zetu tuzioshe,
Kwa damu ya Mwanakondoo, Nuru yetu iangaze
Ndilo agizo la Mungu, ‘Ombeni na mtapewa,
Tafuteni muone mibaraka, mtafunguliwa.’
Refrain
Je ndugu yangu, wajitahidi kuwa na Yesu?
Na Yesu maishani mwako? (Na Yesu)
Wajitahidi kuwa na amani (Na watu wote)
Upendo wa ukweli hauhesabu baya katika maisha
Sote ni ndugu katika Kristo,
Twahitaji msaada wa Mungu.
2. Sasa tunamjua Mungu, hakika tutashinda
Ushindi na Yesu ni wa hakika, Ulielewa urejee
Nguvu kutoka mbinguni, Tumaini lenye heri
Na utakuwa huru kweli, uonapo majaribu
Uliyekata tamaa, Mungu wetu wa upendo
Ndiye ajuaye yajayo mbele, asihi urudi.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 29, Bedi Score, Bedi Lyrics