Friday, 8 May 2026

Watu wanahangaika (Amani) Lyrics, Songs from the Radio

Watu wanahangaika (Amani) Lyrics, Songs from the Radio


1. Watu wanahangaika, wakitafuta amani

kila sehemu ni vita, pia maombolezo

Wamekwenda kwa waganga, na hata kwao wasomi

Lakini wameikosa, amani iko wapi?


Stanza 1 With articulation/2nd Augmenting voice

Watu wanahangaika (Wahangaika), wakitafuta amani (Amani)

kila sehemu ni vita (Ni vita), pia maombolezo (Maombolezo)

Wamekwenda kwa waganga (Waganga), na hata kwao wasomi (Wasomi)

Lakini wameikosa, amani iko wapi? (Amani iko wapi?)


Refrain

Yesu ndiye kimbilio, lenye amani

Tumtafute Mwokozi, tuweze pata amani

Yeye pekee anaweza, kushinda yote

Tukimbilie kwa Yesu tutapata amani.


2. Na katika familia, amani imetoweka

migongano haiishi, watu wanafarakana

Shetani ametowesha, amani kati ya ndugu,

Ndugu umkaribishe, yeye mwenye amani.


Stanza 2 With articulation/2nd Augmenting voice

Na katika familia (Familia),  amani imetoweka (Ooh kweli)

migongano haiishi (Haiishi), watu wanafarakana (Wafarakana)

Shetani ametowesha (ametowesha), amani kati ya ndugu (Amani)

Ndugu umkaribishe yeye mwenye amani (Yeye mwenye amani)


This is from the Radio; Singers not attributed. Attribution could be done later.

2017, Morning Star Radio Tz


Songs from the Radio, Fillers, Attribution Needed, Bedi Score, Bedi Lyrics

Nikitazama Dunia (Ukimwi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nikitazama Dunia ( Ukimwi ) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nikitazama dunia, Inaombolezayo waya waya Magonjwa yenye kutisha, Yanavyowa...