Monday, 8 June 2026

Iligonga Mwamba (Meli Titaniki) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Iligonga Mwamba (Meli Titaniki) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1. Iligonga mwamba, meli Titaniki ikazama

Walokuwa ndani ya meli hiyo walizama

Meli kubwa nzuri ilizama, Titaniki.


Iligonga mwamba meli Titaniki ikazama

Walokuwa ndani ya meli hiyo walizama

Meli kubwa nzuri ilizama Titaniki

Meli kubwa nzuri ilizama Titaniki.


Refrain

Dunia sasa yagonga mwamba,

Ni sawa na Titaniki (Titaniki)

Mashua yetu ni kwake Yesu,

Kimbilio letu, la Wokovu (Haleluya).


2. Meli kubwa nzuri, iliaminiwa kutozama

Iligonga mwamba na ikazama taratibu

Waliokuwa ndani yake, walizama.


Meli kubwa nzuri iliaminiwa kutozama (lakini)

Iligonga mwamba na ikazama taratibu

Waliokuwa ndani yake walizama

Waliokuwa ndani yake walizama.


3. Dunia ya leo, yafanana nayo Titaniki

Itateketezwa na wote waliomo ndani

Mashua pekee ya Wokovu, ndiye Yesu.


Dunia ya leo yafanana nayo Titaniki

Itateketezwa na wote waliomo ndani

Mashua pekee ya Wokovu ndiye Yesu

Mashua pekee ya Wokovu ndiye Yesu.


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir Assorted, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics

Nikitazama Dunia (Ukimwi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nikitazama Dunia ( Ukimwi ) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nikitazama dunia, Inaombolezayo waya waya Magonjwa yenye kutisha, Yanavyowa...