Mbingu Zilikaa Kimya (Kutafuta Mkombozi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Mbingu zilikaa kimya kwa masikitiko makubwa,
Kutafuta Mkombozi wetu atakayetuokoa (kwani)
Kwani tulipotea bila tumaini la Wokovu
Hakuna aliyejibu, “Nipo Bwana wangu unitume.”
Refrain
Tumepata Mkombozi, Yesu mwana pekee, Kutoka kwa Baba yake
Kamwe tusiwe na hofu, Mkombozi wetu ni Yesu Kristo
Kamwe tusiwe na hofu, Mkombozi wetu ni Yesu Kristo.
2. Ndipo Yesu akasema, “Nipo Bwana wangu nitume
Ntaondoka niende nikawatafuta walopotea
Na wakilia wote wenye dhambi wapate uzima,"
Kwa pendo la agape Yesu kajitoa kutufilia.
3. Tutalipa nini kwa pendo la Yesu, juu Msalabani?
Kwa damu aliyomwaga, watu wote tuokolewe
Sisi, hatuna cha kulipa bali kulifuata neno lake
Ndipo Mbingu zitafurahi mwanadamu kuokolewa.
Kurasini SDA Choir Assorted, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics