Najuta Kwa Kuwazia (Nimeamua Kumfuata Yesu) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Najuta kwa kuwazia,
Maumivu na matatizo ya maisha
Nimepoteza wakati, Kwa kung'ang'ania,
Mambo nisiyoweza.
Refrain
Sitamani mambo ya zamani
Rehema zake kwangu zimenipa furaha
Nasonga mbele naye Yesu yuko nami.
2. Naacha kuwalaumu,
Na kuwachukia watu na matukio
Mzigo wa hatia,
Nimeutua na Yesu kanipa furaha.
3. Nakubali badiliko,
La maisha yangu na mimi natambua
Bwana Yesu amefanya makao,
Ndani yangu, Nimeumbwa upya.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Vol 28, Bedi Score, Bedi Lyrics