Ndugu Unaposema (Ubatizo) Lyrics sung by Diana Gesare
1. Ndugu unaposema kwamba umebatizwa,
Imekupasa kuyachunguza sana maneno yako
Kwani ubatizo una maana ya kuzamisha,
Alivyozamishwa Mwokozi wetu Yesu mtoni Yorodani
Alivyozamishwa Mwokozi wetu Yesu mtoni Yorodani.
Refrain I
Uzamishwa ndani ya maji, maji yalo mengi
Ni ishara ionyesha kufa na kufufuka.
Refrain II
Ndiyo ubatizo ulio wa kweli,
Hebu na tufuate nyayo za Bwana Yesu.
2. Tuna Baba mmoja, Biblia ni moja, Imani moja
Na njia nayo ni moja, ambayo ni Yesu
Mbona tusizifuate nyayo zake Mwokozi?
Kwa kubatizwa alivyobatizwa Bwana Yesu mtoni Yorodani
Kwa kubatizwa alivyobatizwa Bwana Yesu mtoni Yorodani.
3. Ubatizwapo ndugu, kumbuka ni ishara,
Ya kuyazikwa mambo yale ya zamani yalo ya giza
Ebu mwamini leo ufanye uamuzi
Ili uzaliwe mara ya pili uwe kiumbe kipya
Ili uzaliwe mara ya pili uwe kiumbe kipya.
Diana Gesare.
Diana Gesare, Bedi Score, Bedi Lyrics