Kisa Cha Msalaba Lyrics sung by Diana Gesare
1. Kisa cha Msalaba chagusa moyo wangu,
Alivyoteseka kwa ajili yangu
Taji ya miba alivikwa Bwana wangu,
Ili mi' na wewe tupate kuokoka.
Refrain
Machozi ya Mwokozi yazidi kutiririka,
Anapotuona tukipotea dhambini,
Anatuita leo kwa sauti ya upole
Fungua moyo aingie.
2. Njiani Goligotha alitembea Bwana
Msalaba mzito ukamlea,
Mkuki ubavuni alichomwa Bwana wangu
Mikononi, miguuni kachomwa misumari.
3. Leo Yesu Mwokozi yu mlangoni mwako,
Akusihi ndugu umpokee maishani
Kwani gharama yetu ya Wokovu alilipa,
Njoo nami leo hii tumfuate Mkombozi.
Diana Gesare.
Diana Gesare, Bedi Score, Bedi Lyrics