Yesu Akiwa Ni Kiongozi Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Pre-Verse
Mambo yako sawa
Nifike salama. ×1
1. Sitahofu safari, japo ni ngumu
Yesu pamoja nami,
Ataangaza njia nitembeapo,
Ili nisijikwaye. ×2
Refrain ×2
Kaza mwendo (ndugu) utafika
Angaza macho yako kwake Yesu
Ndiye nuru hakika ya kweli.
2. Basi njooni sote tuandamane,
Makao yatungoja
Kwa imani, sala naye Yesu,
Mbinguni twaiona. ×2
Refrain ×4
Usitie shaka msafiri
Kaza mwendo (ndugu) utafika
Angaza macho yako kwake Yesu
Ndiye nuru hakika ya kweli.
Outro
Yesu akiwa ni kiongozi,
Mambo yako sawa
Mapito yangu atayanyosha,
Nifike salama. ×1
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Assorted, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics