Thursday, 12 June 2025

Nani Kati Yenu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1. Nani kati yenu mtoto akimwomba mkate,
Yeye kama mzazi---atampa jiwe?
(Hum*3) Nani kati yenu mtoto akimwomba samaki,
Yeye kama mzazi---atampa nyoka?
(Hum*3) Baba wa mbinguni ni Baba anayetupenda
Mahitaji yetu---ajua ya kesho
(Hum*3) Anasema bisha malango ya mbinguni wazi,
Kila abishaye---atafunguliwa

Pre Chorus
Ameahidi baraka tele, Na ahadi zake ni za kweli
Msiwaze mambo ya kesho, yeye ayajua
Njooni kwake kwa ujasiri, Na enyi nyote mliolemewa
Msiwaze mambo ya kesho, yeye ayajua

Chorus
Tunajivunia Yesu, nani kama wewe?
Baba anayejua kutunza, analea
Mahitaji yetu yote mikononi mwake,
Hakika, (na) atupenda
Ni lini ‘tafika kwake nimwone uso kwa uso?
Yesu (Yesu), atupendaaa…

2. Ninajivunia jina la Yesu la thamani,
Kwake ninapata---uzima milele
(Hum*3) Ninajivunia simba wa kabila la Yuda,
Kivulini mwake---napata faraja
(Hum*3) Kila nikimwita yu tayari kunisikia,
Yuko ndani yangu---nami ndani yake
(Hum*3) Anasema bisha malango ya mbinguni wazi,
Kila abishae---atafunguliwa.

Kurasini SDA Choir.

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...