Njooni Kwenye Kisima Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Njooni Kwenye Kisima Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Njooni kwenye kisima cha Bwana, Kuna maji ya uzima tele
Nyote mliojawa na kiu, Njooni kwenye kisima cha Bwana
Atakayekunywa maji ya kisima, Kisima cha Mwokozi
Hataona kiu milele milele
Refrain
Usikiapo sauti ya Bwana, Fanya hima uje leo kwenye kisima
Upate maji ya uzima bure bure-bure, Yanayotolewa na Yesu bure
Na wale wanaotaka kuoga, Watakuwa wasafi wana wa Mungu
Njooni nyote katika kisima, Muoge na kunywa bure
2. Wito wa Yesu ni kwa watu wote, ‘Njooni kwangu mliochoka
Na mliolemewa na dhambi, Nira yangu ni laini njooni
Tena mzigo wangu kwenu ni mwepesi, Njooni mpumzike
Nitakuwa nanyi mwisho wa dahari.’
Kurasini SDA Choir.