Tunaye Roho - Anatuombea Lyrics sung by Acacia Singers
Tunaye Roho - Anatuombea Lyrics sung by Acacia Singers
1. Tunaye roho wake Mungu, Ambaye ni msaidizi
Hutuongoza kwenye ukweli, Hata tusitende uovu
Roho wa Mungu tuliyepewa, Hutukumbusha maagizo
Roho wa Mungu tuliyepewa, Hutukumbusha maagizo
Refrain
(Na bado) Anatuombea,
Juu mbinguni
(Na bado) Anatuombea
Dhambi zetu zipate kufutika
2. Tunaye mwana Yesu Kristo, Anatuombea kwa Baba
Hutuongoza kwenye kweli, Mchunga mwema wa kondoo
Mwombezi wetu kule mbinguni, Mtetezi wa wenye dhambi
Mwombezi wetu kule mbinguni, Mtetezi wa wenye dhambi
3. Lishike neno lake Mungu, Ukadumu kwenye sala
Naye roho mtakatifu, Atakujaza nguvu tele
Roho wa Mungu tuliyepewa, Usimuache aende zake
Roho wa Mungu uliyepewa, Usimuache aende zake
4. (Solo)
Mpatanishi, Yesu Kristo, Yeye aliye na mauwa
Kuhani wetu mwenye haki, Mtakatifu wake Bwana
Mwanakondoo aliyechinjwa, Kwa ajili ya wenye dhambi
Mwanakondoo aliyechinjwa, Kwa ajili ya wenye dhambi
Refrain
(Oh, Na bado) Anatuombea
(Kule kwa Baba) Juu mbinguni
(Kweli bado) Anatuombea
Dhambi zetu zipate kufutika
Refrain
(Nasema bado) Anatuombea
(Kule kwa Baba) Juu mbinguni
(Kweli bado) Anatuombea
Dhambi zetu zipate kufutika
Outro
Dhambi zetu; zetu zipate kufutika
Dhambi zetu; zetu zipate kufutika
Dhambi zetu; zetu zipate kufutika
Dhambi zetu; zetu zipate kufutika.
Acacia Singers.
For Revision
#ForRevision
?kweli/ukweli