Nitasimulia Kisa Cha Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nitasimulia Kisa Cha Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

1. Nitasimulia kisa cha Yesu,
Kwa matendo makuu aliyotenda
Kwa rehema zake nitasimulia,
Amebadilisha maisha yangu
Sasa natambua kwamba anipenda,
Nitasimulia habari zake
Kamwe sitaacha kunena habari,
Habari za Yesu tamu kwangu

Pre-Chorus
Nitasimulia habari zake,
Amebadilisha maisha yangu
Nilikuwa vile leo niko hivi,
Amebadilisha maisha yangu
Nitasimulia habari zake

Chorus
Mashariki (wote) kusini, wasikie
Kaskazini (wote) magharibi, wasikie (wasikie)
Vilindini (wote) na bahari, wasikie
Juu angani viumbe viseme ya kwamba Yesu;
Mfalme wa utukufu

2. Katika tanuru amenilinda,
Tunduni mwa simba kashuka kwangu
Amenikingia mauti juu yangu,
Hukumu ya kifo aliibeba
Sasa natambua kwamba anipenda,
Nitasimulia habari zake
Kamwe sitaacha kunena habari,
Habari za Yesu tamu kwangu.

Kurasini SDA Choir.

#RepeatPostedLyrics Second Time Posting.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Muumbaji Mfalme Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA