Bwana Neno Lako Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Bwana neno lako lasimama,
Imara mbinguni hata milele
Neno lako taa ya maisha yangu,
Na tena mwanga wa njia yangu
Refrain
Hebu nena nami Bwana, Niko tayari kusikia
Nitashukuru kwa wema wako, Usiniache nipotee
Fadhili zako zinifikie, Eh Bwana ninakuhitaji
Fadhili zako zinifikie, Eh Bwana ninakuhitaji
2. Nimeyachoka maisha ya uasi,
Tuokoe Bwana tunakusihi
Tutambue njia ya uaminifu
Majaribu yote tutayashinda.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 33, Bedi Score, Bedi Lyrics