Chukua Tahadhari Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Verse 1
Chukua tahadhari, Rejea kwake Mwokozi wako (Angojea)
Tazama akusihi moyoni mwako mfungulie
Daima mashakani atakulinda usione shida
Tua mzigo wako kwake Yesu, Tua matatizo yako
Toa moyo wako ubadilishwe, Kwa damu utakasike
Uhesabiwe mwana wa Kimfalme
Verse 2
Umetanga mbali na Bwana, Mwana mpotevu rudi
Umesongwa na mawazo moyoni mwako hima urejee
Umetanga mbali na Bwana (Rejea),
Mwana mpotevu rudi (Kwake)
Umesongwa na mawazo moyoni,
Hima urejee kwake Bwana,
Nyumbani kuna pumziko
Verse 3a
Ufalme wa Mungu u tayari, (Ufalme u tayari kwa yule)
Tayari kwa yule, Kwa amtafutaye Mungu
Huko ni furaha na amani (Huko ni furaha na amani)
Shida zetu zote zitakwisha ni mambo mapya
Hima urejee kwake Bwana, Nyumbani kuna pumziko
Repeat as above Noting the variation
Verse 1
Chukua tahadhari, Rejea kwake Mwokozi wako (Angojea)
Tazama akusihi moyoni mwako mfungulie
Daima mashakani atakulinda usione shida
Tua mzigo wako kwake Yesu, Tua matatizo yako
Toa moyo wako ubadilishwe, Kwa damu utakasike
Uhesabiwe mwana wa Kimfalme
Verse 2
Umetanga mbali na Bwana, Mwana mpotevu rudi
Umesongwa na mawazo moyoni mwako hima urejee
Umetanga mbali na Bwana (Rejea),
Mwana mpotevu rudi (Kwake)
Umesongwa na mawazo moyoni,
Hima urejee kwake Bwana,
Nyumbani kuna pumziko
Verse 3b (Check line 2 variation)
Ufalme wa Mungu u tayari, (Ufalme u tayari kwa yule)
Tayari kwa yule, Kwa aliyetubu dhambi
Huko ni furaha na amani (Huko ni furaha na amani)
Shida zetu zote zitakwisha ni mambo mapya
Hima urejee kwake Bwana, Nyumbani kuna pumziko
Hima urejee kwake Bwana, Nyumbani kuna pumziko.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 32, Bedi Score, Bedi Lyrics