Ole Ole Inakuja Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Ole! Ole! Inakuja, Ole kutoka mbinguni
Changamkeni wokovu u mlangoni
Dunia itaachwa ukiwa siku inakujaa kilio kusaga meno
Mambo yote tunayoyaona yale tunayoyapenda yote tutayasahau
Ndio sababu ninasimama njia panda nikipaza sauti (Ooh-Ooh)
Ndio sababu ninasimama njia panda nikipaza sauti
(Kwenye) Nasimama kwenye njia panda
Ninasimama nikipaza sauti (Ooh-Ooh)
Waendao wasikie kotekote
Wasikie habari za wokovu
Kama Yona alivyopiga kelele
Watu wa Ninawi wakamsikia
Hizi ni habari za wokovu (Ooh-Ooh)
2. Kwa ujasiri nasimama njia panda
Natangaza kotekote injili ya marejeo
Kabla lango la rehema halijafungwa kwa wote waliodharau wito
Nafasi kwa watu wote bado ii wazi fanya matengenezo sasa harakisha
Ndio sababu ninasimama njia panda nikipaza sauti (Ooh-Ooh)
Ndio sababu ninasimama njia panda nikipaza sauti
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 31, Bedi Score, Bedi Lyrics