Tumwimbie Sifa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Tumwimbie sifa tena wote na tumwabudu
Pembe zote za dunia umezishikilia wewe
Utukufu sifa zikurudie Bwana
Mamlaka na nguvu zote ni vyako ewe Bwana
Refrain
Haleluya Bwana, Nani kama wewe?
Malaika wote wanakusifu Mfalme
Hata sisi leo tunakuinua
Tutakuimbia Mungu Bwana wa mabwana
2. Malaika wote maserafi na makerubi
Na viumbe vyote Bwana hakuna wakufanana nawe
We ni mkuu mno watu wote wajue
Ndio maana twaimba sifa wewe Alfa na Omega.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Vol 32, Bedi Score, Bedi Lyrics