Wewe Shetani Sikia Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Wewe Shetani sikia tena sikia
Unayo masikio nasema sikia
Wewe una makao hapa duniani
Mimi nina makao kwa Baba mbinguni
Mimi si wako ninaye Yesu
Urafiki wangu nawe watoka wapi?
Nipishe njia naelekea mbinguni (O-Ooh)
Refrain
Wewe ulifukuzwa mbinguni
Na kuhukumiwa kifo milele (Milele)
Maishani mwangu ninaye Yesu
Kwenye shida kwenye raha ni Yesu (Ni Yesu)
Moyoni mwangu nina amani
Amani itokayo kwa Yesu (O-Ooh)
Nasubiri kao jipya (O-Ooh)
2. Wewe Shetani sikia tena sikia
Huna nafasi katika maisha yangu
Hukumu yako bila shaka waijua
Utakinyweya kikombe chako mwenyewe
Huna nafasi moyoni mwangu
Tambua leo ninaye Yesu rafiki
Nipishe njia naelekea mbinguni.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 31, Bedi Score, Bedi Lyrics