Thursday, 7 May 2026

Hapo Kule (Ayubu) Lyrics sung by Acacia Singers

Hapo Kule (Ayubu) Lyrics sung by Acacia Singers


1. Hapo kale kwenye mji wa Usi,

Alikuwepo mtu mmoja, Mkamilifu mtakatifu

Ndiye Ayubu mchaji wa Mungu,

Alikumbwa nayo majaribu, Akapoteza watoto wote

Mali nazo zikateketea,

Ndugu zake wakamkeuka, Lakini alisimama imara

Ndugu zake wakamkeuka, Lakini alisimama imara.



2. Ayubu alimtazama Mungu,

Katika saa ya kujaribiwa, Kwani mkewe alimgeuka

Akataka akufuru afe

Lakini Ayubu hakujali, Hata alipopoteza vyote

Akadumu kumwamini Mungu,

Mwisho Mungu akamwinua, Na kumzidishia tele

Mwisho Mungu akamwinua, Na kumzidishia tele


3. Je ndugu unasumbuka sana?

Na kulemewa na ya dunia, Maradhi vifo, njaa, mateso,

Vyakuandama kila wakati?

Ndugu jamaa wakukimbia? Hata wapoteza tumaini?

Sikia sasa habari njema,

Mtazame Yesu Mwokozi, Atakushindia yote

Mtazame Yesu Mwokozi, Atakushindia yote.


Acacia Singers Tz.


Acacia Singers Tz Mwenge, SDA Swahili Songs, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...