Imani Yangu Haba (Nina Taabu) Lyrics sung by Messengers
1. Imani yangu haba tena ya mashaka
Nashindwa hata kujua hata ya kesho
Nasikia sauti yaniita moyoni
Yanisihi nimtafute Mwokozi
Refrain
(Taabu) Nina taabu ninasumbuka kwenye wimbi
(Kwenye wimbi) Wimbi la mashaka
Nipe nguvu za kushinda vyote
Kristo msaada milele
2. Dhoruba za maisha zikinitikisa
Wakati mwingine ninaanguka
Na kwa mkono wake ninapata nguvu
Ninasimama kumshukuru Yesu.
Messengers
Messengers, Simba Wa Yuda Vol 3, Bedi Score, Bedi Lyrics