Tena Umepata Kusikia (Njoo Nyumbani) Lyrics sung by Messengers
1. Tena umepata kusikia, Pendo lake Yesu, (Ndugu yangu)
Ikinong’oneza moyoni mwako
Unapojipata u pekee yako, Je wapata raha (Ndugu yangu)
Yesu anakuita kwa upole (Kwa upole)
‘Njoo,’ Bwana asema, ‘Njoo (Njoo)’
Mbona wazi, Waenda mbali?
Yesu alijishusha (Shusha)
Kuja kututafuta
Nayo damu yake (Bwana Yesu)
Inatutakasa, Wenye dhambi
‘Njoo mwanangu, Njoo nyumbani’
‘Njoo mwanangu, Njoo nyumbani’
2. Alitoka juu akaja kwetu, Sisi wenye dhambi ndugu yangu
Lakini hao hawakumtambua
Walimwangika pale Kalvari, Bila ya makosa (Ndugu yangu)
Yesu alijitoa tuokoke (Wenye dhambi).
Notes
Chorus, Line 2: Mbona wazi, waenda mbali? (Ni wazi wazi kuwa unaenda mbali, Kwa nini unaenda mbali?)
Messengers
Messengers, Simba Wa Yuda Vol 3, Bedi Score, Bedi Lyrics