Monday, 11 May 2026

Sikuja Na Kitu Hapa Duniani Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Sikuja Na Kitu Hapa Duniani Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1. Sikuja na kitu hapa ulimwenguni,

Hilo nalitambua sababu niliumbwa,

Nitarudi tena huko nilikotoka,

Bila kuwa na kitu, vyote ni vya Bwana


Bwana wangu mimi sina dhamani

Nikumbushe nikutumikie,

Hadi mwisho wa safari yangu, hapa duniani.


Refrain

Sikuja na kitu hapa duniani,

Na vyote nitaviacha duniani

Moyo wangu watosha kwa Bwana aliyenipa vyote

Jambo moja yangu sasa liko mbele yangu

Ni kutangaza marejeo ya Bwana,

Hadi mwisho wa safari yangu, nione utukufu.


2. Wakati mwingine Bwana najisahau,

Huku nikijikweza kwa mambo ya dunia,

Bwana nikumbushe niweze kujishusha,

Kwenye miguu yako nikutumikie,


Bwana wangu mimi sina dhamani

Nikumbushe nikutumikie,

Hadi mwisho wa safari yangu, hapa duniani.


Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 29, Bedi Score, Bedi Lyrics

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya

Wewe Ni Baba (Jenga Boma) Lyrics sung by Majaoni AY Kilifi, Kenya 1. Wewe ni Baba wa kinilinda We ndiye shina anipendaye Marafiki wataponia...