Tafuteni Kila Saa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Tafuteni kila saa kumpendeza Mungu,
Kwetu, Ajuaye shida zetu maishani mwetu
Tafuteni amani nao watu wote,
Faraja na upendo
Unapomlilia Bwana yuko karibu
Unapomlilia Bwana yuko karibu
Refrain
Mwili ni dhaifu lakini jipe moyo
Utapata nguvu toka kwa Yesu
2. Wamtafutao kwa bidii watabarikiwa
Watang’aa kama nyota mikononi mwake
Tafuteni amani nao watu wote,
Faraja na upendo
Unapomlilia Bwana yuko karibu
Unapomlilia Bwana yuko karibu
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 30, Bedi Score, Bedi Lyrics