Bwana Wangu (Nakushukuru) Lyrics sung by Diana Gesare
1. Bwana wangu sijui, Na sina cha kukupa kwa upendo wako
Ulikonitoa hakuna mwanadamu yeyote awezaye kueleza
Lakini kwa upendo wako ulo mkuu, sasa nashukuru.
Refrain
Wakati ule wa giza nene, Moyoni mwangu uliniona eh Bwana
Mimi sikuzitambua njia zako za siri, Nakushukuru Bwana wangu.
2. Sasa nina sababu, ya kulitukuza na kuliinua jina lako eh Bwana
Wakati wa shida u rafiki wa kweli, ambaye namtumainia.
Diana Gesare, Bedi Score, Bedi Lyrics