Ni Machungu Yasononeshayo Lyrics sung by Diana Gesare
1. Ni machungu yasononeshayo, yatukumbayo ndugu
Tupitiayo humu duniani, kweli yanatisha
Wana wa Mungu wateseka, kila aina ya machungu
Lakini jambo moja linipalo faraja kwamba atarudi
Lakini jambo moja linipalo faraja kwamba atarudi.
Refrain
Bwana wangu ninajua atarudi,
Huu mwili unaoteseka sasa utaisha
Nitavikwa mwili mpya,
Nikiingia Yerusalemi mpya pasipo na mateso
Nikiingia Yerusalemi mpya pasipo na mateso.
2. Wengi wajifanya marafiki, lakini yale watutendeayo,
Kweli yanatisha, Tunaye rafiki wa kweli,
Ambaye ni Yesu Mkombozi
Ameshatuahidi ya kwamba, kamwe yeye hawezi kutuacha
Ameshatuahidi ya kwamba, kamwe yeye hawezi kutuacha.
Refrain
Bwana wangu ninajua atarudi,
Huu mwili unaoteseka sasa utaisha
Nitavikwa mwili mpya,
Nikiingia Yerusalemi mpya pasipo na mateso
Nikiingia Yerusalemi mpya pasipo na mateso.
Outro
Tuwakumbuke Meshaka, Shadrak and Abednego,
Waliporushwa motoni, Bwana aliwashindia
Na sisi leo kweli, tukimwamini Bwana
Atatupa nguvu za kuweza kuyakabili.
Usifadhaike tena, moyoni mwako ndugu
Umwamini Bwana atakushindia,
Yale yote upitiayo yeye anaweza
Atakupa nguvu za kuyakabili kuyakabili
Atakupa nguvu za kuyakabili kuyakabili.
Diana Gesare.
Diana Gesare, Bedi Score, Bedi Lyrics