Jihoji (Je Unafanana Na Mwokozi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Jihoji kama wafanana,
Na Mwokozi Yesu Bwana wako
Ni balozi mwaminifu?
Dini yako kweli yapendeza,
Watu na Mungu duniani
Uwe barua yake Mungu
Uwe barua yake Mungu.
Refrain
Je unafanana na Mwokozi wako,
Katika maneno na matendo?
Bahasha kwa juu, anwani ya Yesu
Barua kwa ndani, si ya Yesu.
2. Ukristo wako majira,
Wafanana na wafarisayo
Walijipamba kwa nje,
Siku sita ni kwa ulimwengu,
Sabato ni kwake Mungu Muumbaji
Wasomekaje ndugu yangu?
Wasomekaje ndugu yangu?
3. Uwapo ndani ya Kanisa,
Yesu Mwokozi ni Bwana wako
Ukitoka wamuacha,
Mitani pia safarini,
Wafanana nao ulimwengu
Utubu uje kwake Yesu
Utubu uje kwake Yesu.
For Revision (or Affirmation): R3: Bahasha kwa juu, anwani ya Yesu
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Assorted, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics