Ni Takatifu Sana (Ndoa) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Pre-Verse
Ni takatifu sana kwake Mungu,
Ndoa ya leo sikiliza.
1.Mungu aliona si vyema,
Mtu kuishi akiwa pekee yake
Akampa msaidizi,
Hata leo twashuhudia (Mungu).
Refrain
(Ndoa) Ndoa ni agizo toka kwake Mungu,
Ipewe heshima na watu wote
Maarusi wetu Bwana awe nanyi,
Muyaanzapo maisha mapya.
2. Bwana harusi na bi harusi
Sio wawili bali ni mwili moja
Tendeeni yote kwa pamoja
Bwana Yesu awaongoze (Bwana).
3. Vumilianeni daima,
Uaminifu ni kitu cha maana
Msimruhusu Shetani,
Atawale nyumbani mwenu (Maarusi).
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Assorted, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics