Ni Watano (Walibisha Hodi Hodi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Ni watano, Waliokuwa ni wajinga
Na watano, Walikuwa wenye busara
Wote walisubiri, Bwana harusi pamoja
Wote walisubiri, Bwana harusi Pamoja.
Tazama; na wajinga hawakuwa na akiba; mafuta
Na la kushangaza, Bwana harusi kachelewa.
Tazama; na wajinga hawakuwa na akiba; mafuta
Na la kushangaza, Bwana harusi kachelewa.
Wote wakasinzia, wakalala usingizini
Wote wakasinzia, wakalala usingizini.
2. Usiku wa manane, sauti ikasikika
Bwana harusi amefika, Wote wakatoka usingizini
Kumlaki Bwana harusi, Ole wao wale wajinga
Walikosa mafuta, Taa zao zikazimika.
Usiku wa manane, sauti ikasikika
Bwana harusi amefika, Wote wakatoka usingizini
Kumlaki Bwana harusi, Ole wao wale wajinga
Walikosa mafuta, Taa zao zikazimika.
Refrain
Walibisha hodi, hodi (hodi) tufungulieni mlango
Kwani hata sisi, tumekesha tukisubiri
(Huzuni) Na huzuni ni kwamba (kwamba), hau’funguliwa tena
Ni aibu kubwa, kwamba tutafunguliwa nje.
3. Kweli nyinyi ndio taa, ya ulimwengu wa sasa
Tangazeni ujumbe huu, kwa kukesha ombeni msichoke
Msififie kwa imani, imani ndiyo mafuta
Akiba ni kwa Bwana, aliye Mkombozi wetu.
Kweli nyinyi ndio taa, ya ulimwengu wa sasa
Tangazeni ujumbe huu, kwa kukesha ombeni msichoke
Msififie kwa imani, imani ndiyo mafuta
Akiba ni kwa Bwana, aliye Mkombozi wetu.
Refrain
Walibisha hodi, hodi (hodi) tufungulieni mlango
Kwani hata sisi, tumekesha tukisubiri
(Huzuni) Na huzuni ni kwamba (kwamba), hau’funguliwa tena
Ni aibu kubwa, kwamba tutafunguliwa nje.
NOTES
R(Huzuni) Na huzuni ni kwamba (kwamba), hau’funguliwa tena; (Huzuni) La huzuni ni kwamba, hau-ku-funguliwa tena
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Assorted, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics