Ninapofikiria Bustani Ya Edeni Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Refrain
Ninapofikiria Bustani ya Edeni,
Ilivyopambwa vizuri, Yapendeza macho,
Mito yatiririka, Mambo yote ni mazuri
Mungu akiwapo kati yao kila siku.
Verse
Dhambi ikapendeza na kuharibu Edeni
Utukufu wa Mungu ukatoweka kabisa,
Hofu ikatawala, uovu ukazidi
Ulinzi ukatoweka, bustanini.
Refrain
Ninapofikiria Bustani ya Edeni,
Ilivyopambwa vizuri, Yapendeza macho,
Mito yatiririka, Mambo yote ni mazuri
Mungu akiwapo kati yao kila siku.
Verse (Outro)
Lakini jambo moja niwaambieni mjue
Tutaiona tena Bustani hiyo nzuri,
Iliyojawa na nuru (Ya mbinguni) siku zote
Tutaiona tena Bustani hiyo nzuri,
Iliyojawa na nuru (Ya Mbingu) siku zote.
Tutaiona tena Bustani hiyo nzuri,
Iliyojawa na nuru (Ya mbinguni) siku zote
Tutaiona tena Bustani hiyo nzuri,
Iliyojawa na nuru (Ya mbinguni) siku zote.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Vol 26, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics