Tuesday, 2 June 2026

Tangu Nimjue Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Tangu Nimjue Yesu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1. Tangu nimjue Yesu, Na kumkaribisha moyoni mwangu

Yalopita yamepita, Na kuvaa utu upya ndani yangu

Sijiitaabishi tena, Ya kale hayana nafasi kwangu

Nimevikwa utu upya, Nimekuwa kiumbe ndani ya Yesu.


Refrain

Utu wangu wa zamani, Umezikwa na kuvaa utu upya

Sikumbuki ya zamani, Yesu yu ndani yangu

Nakimbilia Wokovu, Kwa sasa yalopita yamepita

Dunia kwaheri, Yalopita yamepita.


2. Maisha ndani ya Yesu, Ni raha isiyokuwa kifani

Magumu hurahisishwa, Yatoweka kwa jinsi usiyojua 

Mambo yote ya zamani, Hayakumbukwi tena maishani

Mpe Yesu moyo wako, Utaona yote yawezekana.


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir Vol 26, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare

Ndoa Ilibarikiwa Lyrics sung by Diana Gesare 1. Ndoa ilibarikiwa na Mungu , Ilianza pale Edeni Kwani Mungu aliona, si vyema Adamu , Awe pek...