Ungeimba Wimbo Wa Sifa Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
1. Ungeimba wimbo wa sifa, ukimsifu Mungu wetu
Lakini bado hujaimba wa Mwanakondoo,
Ukimsifu Mkombozi ukiwa naye
Lakini bado hujaimba wa Mwanakondoo,
Ukimsifu Mkombozi ukiwa naye.
Refrain
Nitapiga tarumbeta (Tarumbeta)
Nitapiga na kinubi (Na kinubi)
Nitapiga zeze langu,
Kuimba wimbo mpya (Oh Haleluya)
Tulia eh moyo wangu (Moyo wangu)
Tulia katika Bwana (Tulia kwa Bwana)
Tulia moyo wangu, Miguuni pa Yesu.
2. Kinyonge hakitaingia, kuimba wimbo ule mpya
Utengeneza mambo yako, una nafasi
Mapambazuko ni karibu, mfalme aja
Utengeneza mambo yako, una nafasi
Mapambazuko ni karibu, mfalme aja.
Kurasini SDA Choir.
Kurasini SDA Choir Vol 26, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics