Sunday, 14 June 2026

Wengi Wanatamani Lyrics Sung by Kurasini SDA Choir

Wengi Wanatamani Lyrics Sung by Kurasini SDA Choir


1. Wengi wanatamani kumwona Bwana,

Hiyo ni sawa, ni sawa sawa, ni sawa

Lakini neno lasema waziwazi,

Ni kama mtu aliyekimbia simba

Mbele yake akakutana na dubu (dubu mkali),

Siku ya Bwana yawaka kama moto, yatisha.


Refrain

Utavuna kile (kile) ulichokipanda,

Neno la Bwana lasema waziwazi

Uzima milele, au hukumu ya kifo,

Siku ya Bwana yawaka kama moto, yatisha.


2. Siku ya Bwana watu wagawanyika,

Wenye furaha, wenye huzuni, kilio

Kila mtu atabeba furushi lake,

Vilio vingi ndivyo vitavyosikika,

Fanya matengenezo una nafasi, ndugu yangu

Mlango wa rehema ungali wazi, rafiki.


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir Assorted 2, Kurasini Classics, Bedi Score, Bedi Lyrics

Usiku Wa Manane Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Usiku Wa Manane Lyrics sung by Kurasini SDA Choir Pre-Chorus Usiku wa manane , kelele zikasika, Amini; Usiku wa manane, kelele zikasika. Ref...