Thursday, 30 April 2026

Kisha Nikaona Mbingu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Kisha Nikaona Mbingu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


1. Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya

Mara mbingu za kwanza nchi vyote vimeshapita

Nami nikaona Yerusalemi ukishuka

Ukishuka toka kwa Mungu kama bibi harusi

Ukishuka toka kwa Mungu kama bibi harusi


Refrain

Tazama maskani ya Mungu, Pamoja na wanadamu

Mungu ataishi na watu wake, Naye atafuta machozi yote

Maombolezo na maumivu vyote vimekwisha toweka

Maombolezo na maumivu vyote vimekwisha toweka


2. Yeye ashindaye atayaridhi haya milele

Mikono ya Bwana imenyoshwa kwetu atuita

Tuwezeshe Bwana tupokee neema ya Yesu

Tuvishwe utakatifu wake sote kwa imani

Tuvishwe utakatifu wake sote kwa imani.


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 32, Bedi Score, Bedi Lyrics

Nikitazama Dunia (Ukimwi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nikitazama Dunia ( Ukimwi ) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nikitazama dunia, Inaombolezayo waya waya Magonjwa yenye kutisha, Yanavyowa...