Je Umepata Kusikia Habari (Yerusalemi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Verse
Je umepata kusikia habari,
Ya Yerusalemi ukishuka angani?
Je ndugu utakuwepo juu angani,
Yerusalemi ukishuka?
Dunia yanikatisha tamaa, nirudi nyuma
Lakini mimi, sirudi nyuma
Napaa angani, Yerusalemi.
Yerusalemi, utashuka juu angani
Mji wa raha, tutawala na Yesu
Yerusalemi, utashuka juu angani
Mji wa raha, tutawala na Yesu
Refrain 1
Nitaendesha gari la kifalme,
Nitakapofika juu Mbinguni
Nikizunguka kwenye mitaa ya Mbinguni,
Mbinguni kwa Yesu
Usiku mchana hauishi,
Mji ni mzuri wa ajabu
Nitaingia kwa shangwe,
Kwenye mji ule, Mji wake Yesu
Refrain 2
Nitaendesha gari la kifalme,
Nitalivaa joho la kifalme
Mimi nakwenda, sitarudi nyuma
Mimi nakwenda, nakwenda Mbinguni
Nitaziba masikio yangu, nisisikie ya walimwengu
Nisikie sauti ya Yesu, ikisema moyoni mwangu
Nitaziba masikio yangu, nisisikie ya walimwengu (Na)
Nisikie sauti ya Yesu, ikisema moyoni mwangu
Nami nitakaa nyumbani, mwa Baba milele.
Bridge
Yerusalemi, tutaingia kwa shangwe
Tutasahau, masumbuko ya dunia
Yerusalemi, tutaingia kwa shangwe
Tutasahau masumbuko ya dunia
Refrain 1
Nitaendesha gari la kifalme,
Nitakapofika juu Mbinguni
Nikizunguka kwenye mitaa ya Mbinguni,
Mbinguni kwa Yesu
Usiku mchana hauishi,
Mji ni mzuri wa ajabu
Tutaingia kwa shangwe,
Kwenye mji ule, Mji wake Yesu
Refrain 2
Nitaendesha gari la kifalme,
Nitalivaa joho la kifalme
Mimi nakwenda, sitarudi nyuma
Mimi nakwenda, nakwenda Mbinguni
Nitaziba masikio yangu, nisisikie ya walimwengu
Nisikie sauti ya Yesu, ikisema moyoni mwangu
Nitaziba masikio yangu, nisisikie ya walimwengu (Na)
Nisikie sauti ya Yesu, ikisema moyoni mwangu
Refrain 2
Nitaendesha gari la kifalme,
Nitalivaa joho la kifalme
Mimi nakwenda, sitarudi nyuma
Mimi nakwenda, nakwenda Mbinguni
Nitaziba masikio yangu, nisisikie ya walimwengu
Nisikie sauti ya Yesu, ikisema moyoni mwangu
Nitaziba masikio yangu, nisisikie ya walimwengu (Na)
Nisikie sauti ya Yesu, ikisema moyoni mwangu
Outro
Nami nitakaa nyumbani, mwa Baba milele.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 29, Bedi Score, Bedi Lyrics