Monday, 11 May 2026

Kama Wanipenda (Bayona) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Kama Wanipenda (Bayona) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir


Refrain 1

Kama wanipenda,

---------------Simoni Bayona

Kama wanipenda,

---------------Simoni Bayona

Kama wanipenda,

---------------Simoni Bayona

Bayona; Lisha kondoo zangu


Verse 1

Enendeni ulimwenguni mkawafanye,

Watu wote kuwa wanafunzi

Mkawalee mkawatunze, Wasipotee kwenye mikono yenu

Ninatawatuma kama kondoo, kati ya mwitu (Nendeni)

Mimi niko pamoja nanyi, songeni ndani ndani

Vilindini mwa giza, wewe ni nuru safi kwa wengine

Nani aende kuwaokoa? Wito kwa mimi na wewe


Refrain 2

Bayona

---------Simoni Bayona

Kama wanipenda,

---------------Simoni Bayona

Kama wanipenda,

---------------Simoni Bayona

Bayona; Lisha kondoo zangu


Verse 2

Shangwe kubwa vigelegele juu mbinguni,

Malaika wanashangilia, kwa huyo mmoja arejeapo

Kumbuka habari ya mwana mpotevu,

Mkafukue talanta zote mlizozima/ba/pa?

(Fungua) Nyosheni mapito ya Bwana 

Kuna kondoo mmoja analia jangwani, amekata tamaa ya wokovu 

(Kweli) Okoa nafsi ya walioao, Wito ni kwangu mimi na wewe


Verse 3

Amkeni (Amkeni, Amkeni)

Giza la sogea (Giza la sogea)

Machweo karibu, (Machweo karibu)

Amkeni; Wokovu u mlangoni


Amkeni (Amkeni, Amkeni)

Giza la sogea (Giza la sogea)

Machweo karibu, (Machweo karibu)

Amkeni; Wokovu u mlangoni


Outro

Bwana aja na ujira mkononi,

Bwana aja na ujira mkononi.



For Revision: Verse 2, Line 4; Mkafukue talanta zote mlizozima/ba/pa?


Kurasini SDA Choir.


Kurasini SDA Choir, Kurasini Classics, Kurasini Vol 30, For Revision, Bedi Score, Bedi Lyrics

Nikitazama Dunia (Ukimwi) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir

Nikitazama Dunia ( Ukimwi ) Lyrics sung by Kurasini SDA Choir 1. Nikitazama dunia, Inaombolezayo waya waya Magonjwa yenye kutisha, Yanavyowa...