Mwili Huu Ni Dhaifu Lyrics sung by Kurasini SDA Choir
Refrain
Mwili huu wa dhambi, Mwili huu si kitu
Leo wachanua, Kesho wanyauka
Natamani uzima, Uzima milele
Huko nilikotoka, Bwana nirudishe.
1. Bwana alitoa, Bwana atatoa
Mwili huu wa dhambi, sio wa kudumu
Sote tutalala, sote tu mavumbi
Dunia sio kwetu, sote twapita.
Refrain
Mwili huu wa dhambi, Mwili huu si kitu
Leo wachanua, Kesho wanyauka
Natamani uzima, Uzima milele
Huko nilikotoka, Bwana nirudishe.
2. Siku inakuja, tutabadilishwa
Wote waliolala, watafufuliwa
Kufumba fumbua, tutabadilika
Shangwe vigelegele, vitasikika.
Refrain
Mwili huu wa dhambi, Mwili huu si kitu
Leo wachanua, Kesho wanyauka
Natamani uzima, Uzima milele
Huko nilikotoka, Bwana nirudishe.
Kurasini SDA Choir, Kurasini Vol 30, Bedi Score, Bedi Lyrics