Posts

Showing posts from October, 2024

Enyi Msemao/Pasi Yesu Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Enyi Msemao/Pasi Yesu Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Enyi msemao leo kesho tumepanga hii, Leo hiyo, kesho ile, kesho kutwa Mipango yote twahimizwa tumtangulize Mwokozi Refrain Pasi Yesu maishani uzima wetu *ni swali hilo kwetu Maana sisi ni mvuke huonekanao kwa kitambo kidogo Na mwishowe hunyauka hutoweka kabisa  2. Haya basi muusemao tutaingia Mji huu, ule kukaa humo humo kupata faida Pasi Yesu hayo yote ni ya kitambo. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Kweli Sitawaacha/Mungu Ni Mwema Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Kweli Sitawaacha/Mungu Ni Mwema Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Kweli sitawaacha kutangatanga Kama kondoo bila mchungaji Najiandaa kushuka kwenu kuwapeleka Pasipo shida milele zote Mungu ni mwema anatupenda Atashuka chini kutupeleka,* Hatatuacha anatupenda Hatatuacha anatupenda 2. Wana wa Israeli wakienda Kanani Mungu aliwalinda Kwa hivyo uamini akisema atatenda Amini mungu milele zote Cherubim Singers, Nairobi South SDA. *kutupeleka huko juu - Not very clear

Tulia Sikiza/El Shaddai Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Tulia Sikiza/El Shaddai Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Tulia sikiza kwa makini Tunaye Mungu muumba wa vyote Hakuna miungu mwingine twapasayo kuabudu Japo wengine wanaoamini anasa Twambieni yote ni ubatili Japo wengine wanaoamini waganga Twambieni hakuna jibu kwao Refrain Jehova Nissi Mungu wa Israeli, El Shaddai Aitwaye Emanueli Simba wa Yuda Ni nani kama Mungu wetu Ajibuaye maombi yetu Tumsujudu tumsifu Mungu Maana yeye ni Mungu 2. Dunia na vyote vilivyomo Kazi ni yake Mungu muumbaji Tazama alivyotuumba kwa mfano wake Mungu Japo wengine wanateseka kwa magonjwa Twambieni Yesu ni mponaji Japo wengine wanaomboleza mauti   Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Najawa Faraja/Nimechagua Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Najawa Faraja/Nimechagua Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA Chorus Najawa faraja ndani yangu Upendo wako wanishangaza Hauna kipimo haufananishwi Na neema yako Bwana inatuliza moyoni Na fadhili zako (Bwana) siwezi eleza Refrain 1. Nimechagua Yesu wangu Nitakaye mtumikiya Nimechagua Yesu wangu Nitakaye mtumikiya Hata mawimbi yakinipiga pande zote Ninajua nimtumikiaye Atanishika mkono nikianguka Atanitafuta nikipotea Ninapata faraja yuko nami Hajalala usingizi Ninapata faraja yuko nami Hajalala usingizi 2. Bwana tawala ndani yangu Unifanye kiumbe kipya Bwana tawala ndani yangu Unifanye kiumbe kipya Mwovu Shetani hawezi kukushinda Bwana Niongoze kwa (Bwana) njia zako Nitavumilia sitachoka kamwe Nitakaza mwendo sitarudi nyuma Ninapata faraja yuko nami hajalala usingizi. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Dunia Yote Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Dunia Yote Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Dunia yote imekwisha imeoza Twaja mbele zako utupe amani Mungu wetu Refrain Dunia imejaa mahangaiko Twateseka sana Maombi yetu uyasikie Mungu wa rehema Emanueli Alfa na omega twakusihi Mungu wetu 2. Utuongoze safarini duniani hii Shida nazo dhiki mikononi mwako twaziweka Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Gethsemani Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Gethsemani Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Gethsemani usiku ule Bwana Yesu alisumbuka Jasho lake likawa damu Yote, Yote kwa ajili yetu Refrain OOh, Tutaponaje tukikataa Upendo huu wa ajabu Tutaponaje tukikataa Neema hii ya ajabu 2. Msalaba Yesu Mwokozi Alilia kwa uchungu mwingi Akasema eeh Baba yangu Baba, Baba uwasamehe. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Asebayo Mabor Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Asebayo Mabor Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Asebayo mabor kodi Ruodha Yie mond iywaya machiegni kodi buti pile Mak lweta mond iwuoth koda Kiweya dapodhi Yamo malich bende kudho, Obadho ng'eny madi maka Wasigu ng'eny malwora telna e yoo Refrain Nyasacha ine ngimana mochwere Yie mond itelna e pinyni mar mudho Kata e wuodha dute me pinyka Yie mond awuoth kodi Nyasacha Eka mond adonj kodi e ngima, Ngima ma ok norum Ok anyal kenda Ruoth, Yie mond awuoth kodi 2. Yesu nogola e bugo mar richo Modemba gi hera moketa e mor Anawer ng'wonone miwuoro Napake nyaka ji none berne Genona duto ni kuome Ngimana ni e lwete, Onge gima naluor en koda Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Umeinuliwa Juu Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Umeinuliwa Juu Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Umeinuliwa juu Mungu muumba wetu Twataka kusifu jina lako Usitupite ee unastahili sifa na pongezi Sababu ya pendo lako kuu Refrain Kwenye miamba waitwa mwamba wa kale Kwenye wanyama simba wa Yuda kwetu sisi wenye dhambi wewe ni mkombozi Umetuosha umetuweka viumbe vipya  Ndipo tunakusifu tunakuabudu Bwana tunakuinua juu 2. Uwezo na nguvu zote Bwana zatoka kwako Neema hekima zote zako Usitupite ee unastahili sifa na pongezi Sababu ya pendo lako kuu. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Nilikaa Katika Upweke Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Nilikaa Katika Upweke Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Nilikaa katika upweke katika giza la huzuni Nilijaribu kutafakari Juu ya maisha haya upweke Kumbe kando alikuwepo Mungu asikizaye maombi Refrain kwa hii leo amenijibu Ombi hilo nikatisha tamaa Kwa hii sasa nasadiki Mungu hakawii 'timiza ahadi 2. Pengine umeshasumbuka Na moyo umeshavunjika Kila uendako ni giza tu Natumai' limeshatoweka Fikiria Yesu alivyo omba Yakatoka matone ya damu 3. Moyo wangu *umetulizwa Sina hofu juu ya faraja kwa hii wewe ndiwe kimbilio Na wokovu wa maisha yangu Shida taabu zinisongapo Nitaku tazama Mwokozi Cherubim Singers, Nairobi South SDA. *umetulizwa = Not very clear. ?umejulizwa

Pinywani Aneno Orumo Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Pinywani Aneno Orumo Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Pinywani aneno orumo Nyithiwa tang'uru kode Mago mane Yesu owacho koro timore Jonabi duto nokoro ndalo giko piny nonjawni Yiero otayi itang'ne mirimb Nyasaye Owadwa bii ir Yesu, Mondo owari kendo opwodhi Mondo iikri ne biro mare, Mondo wadhiye e dala Zayun 2. Nyithiwa weuru richo dika polo obayi nono Yesu mawuon oganda koro osayoyi Dhood ng'uono ibiro lor Owadwa no yudi kune? Yie kuom Yesu icham gikeni me polo Yie kuom Yesu icham gikeni me polo. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Ruoth Yesu Akwayoi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Ruoth Yesu Akwayoi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Ruoth Yesu akwayoi ipara chieng' giko piny Ka nyinga nobedie bug ngima Anapaki nyaka chieng' Ka nyinga nobedie bug ngima Anamor gi chunya te Eka nakaw thumbe mag locho, Eka nawer wende locho Anapaki Ruodh oganda, Anadendi nyakachieng' Anakaw thumbe mago Anadendi nyakachieng' Anapaki Ruodh oganda, Anadendi nyakachieng' Anakaw thumbe mago, Anadendi nyakachieng' 2. Ananeno masichi Ruoth kiwiro chieng' giko piny Kibiro tieko joma richo Yesu yie mond iwar Aol gi piny aol gi richo Resa e masicheni 3. Aneno dala Nyasaye moseikne joma ler Jerusalem dalano maler moseikne jolocho Agombo dak kanyo mosiko nyaka chieng' Haleluya. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Uwe Nuru Kwa Mataifa Yote Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Uwe Nuru Kwa Mataifa Yote Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Uwe nuru kwa mataifa yote Nuru yenu iangaze kwa watu wote Mungu apate kutukuzwa Mungu apate kutukuzwa Refrain Matendo yenu yawe mazuri Kwa upendo na huruma yenu [siku zote] Popote uwe kielelezo bora Mungu apate kutukuzwa Mungu apate kutukuzwa 2. Muwe chumvi ya ulimwengu Kila siku mkitenda yaliyo mema Mungu apate kutukuzwa Mungu apate kutukuzwa. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Amka Mwenzangu Amka Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Amka Mwenzangu Amka Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Amka mwenzangu amka Amka Mwokozi asema Akusihi ndugu yangu amka Uwe chombo ueleze injili Refrain Wakati ndiyo huu mwenzangu amka Mwokozi akusihi Ueleze injili Ili arudipo mwenzangu [Bwana] Tukamlaki mawinguni 2. Amka mwenzangu amka Amka Mwokozi asema Pambano kuu karibu kwisha Uwe chombo eleze injili. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Yesu Mwokozi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Yesu Mwokozi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Yesu mwokozi Yesu mwokozi Nakulilia mimi mwenye dhambi Na kwa sababu ya unyonge wangu Bwana Naja kwako Bwana unirehemu [Asante] Asante kwa kunikomboa mimi kwa damu yako na dhamani [Bwana] Nilinde ni wako Bwana wangu Niwe chombo kamilifu kwako 2. Japo dhoruba zijatusonga Twaegemea kwako ewe Bwana Wewe ni ngome na kimbilio letu Mwamba uliye imara daima 3. Ahadi zako ni za milele Twatazamia kuja kwako Bwana Ili tuende nawe kule mbinguni Tukaishi nawe siku zote. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Msalabani Pa Mwokozi sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Msalabani Pa Mwokozi sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Msalabani pa Mwokozi Hapo niliomba uzima, Moyo wangu ulitakaswa, Na asifiwe Refrain Na asifiwe, Na asifiwe, (Na asifiwe) Alinikomboa kwa damu yake, Na asifiwe 2. Chini ya mti msumbufu Hapo niliomba amani, Alinikomboa kwa damu, Na asifiwe 3. Damu ya Yesu ya thamani Huniokoa dhambini; Huniendesha wokovuni, Na asifiwe. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Ahadi Tamu Kwa Wanaoamini Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Ahadi Tamu Kwa Wanaoamini Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Ahadi tamu kwa wanaomini Tazama naja upesi sana Uwe imara shujaa msalaba usilale ahadi ukeshe Refrain Na uhifadhi imani yako Nchi mpya itatolewa Njoo ingie rahani mwangu Milele hata milele  Yuaja angani anasimama 2. Tunategemea neno lako Linalotangaza kuja kwako Tumaini letu ni ahadi naja Usilale hadi ukeshe Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Someday The Silver Chord Will Break Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Someday The Silver Chord Will Break Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Some day the silver cord will break, And I no more as now shall sing; But oh, the joy when I shall wake Within the palace of the King! Refrain And I shall see Him face to face, And tell the story, Saved by grace; And I shall see Him face to face, And tell the story, Saved by grace 2.  Some day my earthly house will fall, I cannot tell how soon ’twill be; But this I know– my All in All Has now a place in heav’n for me 3. Some day, when fades the golden sun Beneath the rosy-tinted west, My blessed Lord will say, “Well done!” And I shall enter into rest 4. Some day: till then I’ll watch and wait, My lamp all trimmed and burning bright, That when my Savior opes the gate, My soul to Him may take its flight. Cherubim Singers, Nairobi South SDA. Written by Fanny Jane Crosby

Siku Sita Fanya Kazi #Sabato Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Siku Sita Fanya Kazi #Sabato Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Siku sita fanya kazi Sabato ya Bwana ii karibu Na ya saba uheshimu sabato takatifu Refrain Sabato ni siku gani? [Ooh-ooh] Ni siku ya kupumzika Twendeni sote kwa Bwana Yeye pekee atosha Tumshukuru Mungu kwa kuwa yeye ni mwema siku zote Alitupa uwezo kushinda majaribu yake shetani Sabato takatifu tulioaliandaliwa 2. Enyi ndugu zangu mjiepusha Na anasa za dunia hii Hayana faida tutafute taa ya uzima wa milele Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Nena Mungu sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Nena Mungu sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Nena rohoni Yesu, Nena kwa upole  Sema kwangu kwa pendo, “Huachwi upweke.” Fungua moyo wangu, Nisikie mara; Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana. Kila siku unene, Vile kwa upole. Nong’oneza [kwa pole] wa upendo: “Daima utashinda, Uhuru ni wako.” Nisikie maneno: “Huachwi upweke.” 2. Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia, Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba; Wajifunze kutoa, Maisha kamili, Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi. 3. Nena kama zamani, Ulipoitoa Sheria takatifu: Niiweke pia; Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu, Mapenzi yako tena, Daima kusifu. Cherubim Singers, Nairobi South SDA. F. Campana as Writer, Adapted by Leander Lycurgus. From Nyimbo Za kristo 013

We Shall Sing Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

We Shall Sing Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. We shall sing a mighty chorus over in that glory land We shall join the mighty choir over there Singing of redeeming love marching all around the throne We shall sing to the King Refrain Wondrous singing in heaven with the glorious band What a singing that no one else can compare Angels singing Glory! Glory! to the King What a wondrous joy to be there 2. 'Tis the song of Moses and the song of Holy lamb 'Tis the song that will wipe away our tears Singing there forever more with the sweetest melody We shall sing to the King Cherubim Singers, Nairobi South SDA. Revelation 5:12 Saying with a loud voice, Worthy is the Lamb that was slain to receive power, and riches, and wisdom, and strength, and honour, and glory, and blessing.

Ulimwengu Siutaki Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Ulimwengu Siutaki Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Ulimwengu siutaki Namtaka Bwana Yesu Dunia hunidanganya Yesu yu mwaminifu Refrain Neno la ajabu Taarifa* ya ajabu Pendo bila kipimo Yesu anipenda (anipenda) Kwa pendo la ajabu Ulimwengu siutaki kabisa Nipe Yesu wa milele Ulimwengu siutaki Nipe Yesu wa milele. 2.  Kati ya dhoruba kali Yeye wimbo mtamu Safarini duniani Yeye furaha yangu 3. Ulimwengu siutaki Namtaka Bwana Yesu Msalaba naamini Hata namwona Yesu Nyandema SDA Choir. Taarifa* - The word sung here is not very audible.

Ruoth Yesu Oluongowa Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

 Ruoth Yesu Oluongowa Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Ruoth Yesu oluongowa mond' wadhiye kiserane Molosoni jolocho gini mor manyakachieng' Refrain Koro adhiyo ok adwa deko Nikech Yesu emaluonga We adhi nyak' awinj Ruodha Soprano: Owadwa bii...Nyaminwa bii Alto/Lead Tenor:...adhiyo...adhiyo... All voices(SATB): Wadhii e dalano Bass: Humming; Uuuhm All voices(SATB): Kama kuyo ok nobedie 2. Chieng'no ka tung' noywagi jomothoo duto nochier  Wanago 'riti ne piny jopinywa we uru adhii Outro All voices(SATB): Humming; Uuuhm Lead Oratorio: Yesu Jakwath madieri en emo luongowa mondo wadhi kode dala Nang'o pod igalori e richo to ndalo orumo? Yaye jowadwa, waduog uru ir jawarwa mondo oterwa dala. AAmin All voices(SATB): Kama kuyo ok nobedie. Nyandema SDA Choir. Bible Texts 1Th 4:13 ¶ But I would not have you to be ignorant, brethren, concerning them which are asleep, that ye sorrow not, even as others which have no hope. 1Th 4:16 For the Lord himself shall descend...

Nakaza Mwendo Bwana Uniongoze Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Nakaza Mwendo Bwana Uniongoze Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Nakaza mwendo mbinguni, Kila siku napanda juu; Naomba nikisafiri, "Bwana uniongoze - juu" Refrain Bwana uniinue juu Kwa imani hata mbinguni Juu kuliko dunia; Bwana uniongoze - juu 2. Nataka kupanda juu, Nisishindwe na adui; Kwa imani nasikia Sauti ya washindaji 3. Kupanda juu nataka Niuone utukufu; Hata mwisho nitaomba, "Bwana uniongoze - juu." Outro Bwana uniongoze kwa imani hata mbingu. Nyandema SDA Choir. Bible Text Psalms 31:3 For thou art my rock and my fortress; therefore for thy name's  sake lead me, and guide me.

Kang'iyo Taneno Chandruok Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Kang'iyo Taneno Chandruok Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Kang'iyo t'aneno chandruok jowadwa E ndalogo magiko maduong' mabiro Mago madongo manokor okadho Eno bedi malich owadwa e chieng'no Refrain Ni ere kaka nadagi, nabedi? e chieng'no yawa Ni ere kaka nachungi? e chieng'no mar giko [1. Apenjo] [2. Owadwa] [3. Nyaminwa] [4. Wan waduto] 2. Ni ere ranyisi mapod urito ka tho nitie ka umbe lwenje uwinjo Kech*+, kod* jonabi mag iriambo sani wanenogi kagiwito rombe. Nyandema SDA Choir. Matthew 24:33  So likewise ye, when ye shall see all these things, know that it is near, even at the doors. Mt 24:32 ¶ Now learn a parable of the fig tree; When his branch is yet tender, and putteth forth leaves, ye know that summer is nigh

Hatujui Saa Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Hatujui Saa Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Hatujui saa ya kuja kwa Bwana Yesu, Lakini dalili zasema hivi karibu Atakaporudi na ufalme wake Lakini kwa kweli Hatujui saa yake Refrain Atakuja, kwa vile tukeshe na kuomba; Atakuja Mwokozi, Haleluya! Atakuja kwa fahari ya Baba yake, Hatujui saa ya kuja kwake Kristo. 2. Pana nuru kwa wale wapendao haki, Pana kweli katika chuo chake Mungu; Unabii hufundisha kuja kwake Bwana, Lakini hatujui saa yake Kristo.   3. Tutakesha na tutaimba daima ndugu, Tutafanya kazi mpaka akija Bwana, Tutaimba na tutasoma ishara zake, Hatujui saa ya kuja kwa Mwokozi. Nyandema SDA Choir. Re 22:12 And, behold, I come quickly; and my reward is with me, to give every man according as his work shall be. Re 16:15 Behold, I come as a thief. Blessed is he that watcheth, and keepeth his garments, lest he walk naked, and they see his shame. Mt 25:13 Watch therefore, for ye know neither the day nor the hour wherein the Son of man cometh.

Aliye Na Yesu Rohoni Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Aliye Na Yesu Rohoni Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Aliye Na Yesu rohoni Ana bahati ya uzima wa milele Kwa maana Yesu akirudi Wataridhi ufalme ule wa Bwana Refrain Na sasa Yesu anaita Sauti ya upole Asimama mlangoni We ndugu fungua Ni nani aliyetayari Kumpokea Mwokozi? Ili siku Bwana akirudi Wataingia naye rahani. 2. Heri ni wale wasafiri Ambao wamegundua Yesu maishani Watasafiri salama katika Safari ingawa iwe ndefu Nyandema SDA Choir.

Katika Damu Ya Mwanakondoo Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Katika Damu Ya Mwanakondoo Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Katika damu ya mwanakondoo, Nimeoshwa! Nimeoshwa! Zimeondolewa dhambi zangu, Dhambi zote! Dhambi zote!  Refrain 1 Mimi nilikuwa mwovu kweli, Niliposhindwa na dhambi zangu Sasa damu ni ya Mwanakondoo, Nimeoshwa! Nimeoshwa! (Zangu) 2. Mashaka yangu yametolewa, Nimeoshwa! Nimeoshwa! Hofu ya kufa sinayo leo, Ni salama! Ni salama! Refrain 2 Ingawa sijafahamu yote, Lakini Yesu Mwokozi wangu Na leno lake nagetemea, Ni salama! Ni salama! (Wangu) 2. Wengi wakinidharau sana, Sitarudi! Sitarudi! Nitawaambia watu wote, Wokovu huu! Wokovu huu! Refrain 3 Aniongoze Mwokozi Yesu, Wengi wajue ni wake Bwana Nitawambia watu wote, Wokovu huu! Wokovu huu! (Bwana) Nyandema SDA Choir. 1Jo 1:7 But if we walk in the light, as he is in the light, we have fellowship one with another, and the blood of Jesus Christ his Son cleanseth us from all sin

Pale Mlimani/Wakampiga Wakamtesa Mwokozi Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

 Pale Mlimani/Wakampiga Wakamtesa Mwokozi Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Pale mlimani msiituni Yesu aomba kwa ajili yetu 'Eh Baba yangu niondolee kikombe hiki si kwa mapenzi yangu' Refrain Wakampiga wakamtesa Mwokozi wetu kwa ajili yetu Yesu akasema; 'Eh Baba yangu uwasamehe makosa yao' 2. Walipofika fuvu la kichwa wakayagawa mavazi yake Yesu akasema; 'Eh Baba yangu uwasamehe makosa yao' 3. Wakamtesa Mwokozi wetu/wangu  msalabani akatunikwa Kichwani mwake wakamvisha taji ya miiba Mwokozi wangu. Nyandema SDA Choir. Spiritual Texts It would be well for us to spend a thoughtful hour each day in contemplation of the life of Christ. We should take it point by point, and let the imagination grasp each scene,especially the closing ones. DA 83.4

Tunakusanyika Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Tunakusanyika Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Tunakusanyika kwa pamoja Kulitukuza jina lake Wakerubi japo kundi ndogo Bwana ametuita kwake Twasubiri tena twangojea Siku iliyo ya fahari Tunyakuliwe sote kwake Twende juu  Chorus Tuimbe tusifu wokovu wetu umewadia Pamoja viumbe tumsifu Yesu mwokozi Kitini pa enzi twajongea palipo utukufu mwingi Twakuabudu Mungu Mwenyezi wastahili 2. Utukuzwe kwetu ewe Mungu Nuru yako uiangaze Neno lako liwe ndiyo taa Tunyoshe mapito yako Ufungue Bwana macho yetu Tuweze kukufahamu we Tuhutumie milele Hata juu. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Nilipokuwa Dhambini Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Nilipokuwa Dhambini Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Nilipokuwa dhambini sikujua ni nani atakaye nitoa dhambini Hata marafiki wengi walinikemea Duniani ikaja shida kote Refrain Yesu pekee kanyanijia dhambini kanitoa Ninaye Yesu rafiki mwema Mimi wake yeye mwangu Kivulini mwake nina raha bila Yesu ni bure 2. Ndipo nikagundua ni Yesu pekee atakayenitoa dhambini Sasa nina raha ninaye Yesu atakaye nilinda milele Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Nira Ni Nyepesi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

 Nira Ni Nyepesi Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Nira yangu ni nyepesi mno asema Mwokozi Yesu Bwana wetu wa amani Atakayejitwika nira ya mwokozi Atapata amani moyoni Chorus Alizibeba dhambi zetu pale msalabani alitwikwa Atakutusafi toka kwenye mauti sisi wadhambi tulolemewa Ndiposa leo nafurahia wokovu aloleta Mwokozi mpendwa Ndiposa leo nafurahia wokovu aloleta Mwokozi mpendwa 2. Njooni wote mliolemewana dhambi Kwake mwokozi yesu wetu wa amani Atawapa nira yake ile nyepesi Mkapate amani moyoni. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

Bwana wa mabwana Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. Bwana wa mabwana hatendi jambo Bila kujulisha manabii wake Hata siri ya siku za mwisho kawajulisha Twayaona twasikia dalili hizi Refrain Na dhambi zako umezikalia Zikawa kama hali ya maisha Mahubiri yote umeyasikie Ya kila aina badiliki Kumbuka siku zetu zimeisha Simba wa yuda yuaja mawinguni 2. Hebu we fanya matengenezo yako Kuja kwa Bwana Yesu u karibu Yawezekana usiku hata mchana Akute u tayari kumpokea. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

Winjuru Tinde Kuom Tho Mar Yesu Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

 Winjuru Tinde Kuom Tho Mar Yesu Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Winjuru tinde kuom tho mar Yesu Neen ng'at makare notho nikech an Mondo kuom thone ayudi ngima Adak* mosiko kuom tho mar Yesu Refrain Ayie kuom tho mar Yesu Omiyo an gi ngima Ngima Yesu osimbo mara 2. Ne an jaricho mano oselal chuth Kuom tho mar Yesu angima koro Ngima ma ango en ngima Yesu Erokamano kuom tho mar Yesu 3. Kuom tho mar Yesu adhiye ngima Dala mosiko en Jerusalem Wanane Yesu gi duong'ne polo Erokamano kuom tho mar Yesu Nyandema SDA Choir. Adak* Was not initially clear from my side Adak: "I Now Live" forever because of the death of Jesus Christ. I gain eternal life because of His death.

Mfalme Aliota Ndoto Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

 Mfalme Aliota Ndoto Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Mfalme aliota ndoto yenye Sanamu ya kutisha ndizo falume zote Na Danieli mtu wake Mungu alifunuliwa ndoto ile Refrain Falme zote zitaanguka Zitapita na zitatoweka Wanaojua siri hii Wameweka tumaini kwake Yesu 2. Zilikuwepo falme zenye nguvu Mfano wa dhahabu, wa shaba na chuma Na hizi zote zilishatoweka Na falme zetu zitatoweka 3. Jiwe lililovunja falme zote ni Yesu Mwamba wetu mfalme wa amani Yeye ni mwanzo tena ni mwisho Ufalme wake ni wa milele. Nyandema SDA Choir. Great light shone forth from Daniel and his companions. Glorious things were spoken of Zion, the city of the Lord. Thus the Lord designs that spiritual light shall shine from His faithful watchmen in these last days. If the saints in the Old Testament bore such a decided testimony of loyalty, how should God's people today, having the accumulated light of centuries, shine forth, when the prophecies of the Old Testament shed their veiled glory into the future (Let...

Dunia Inayumba Yumba Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Dunia Inayumba Yumba Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Dunia inayumba yumba Zaonyesha dalili za mwisho Lakini watu hawajali Wamefumba macho na kuyafunga masikio Refrain Lakini binadamu amekataa kabisa kusikia wito wa Mwokozi Yesu Amefumba macho na kuyafunga masikio [Tunaitwa] Tujeni kwa Yesu leo atutakase kwa damu yake  iliyotiririka msalabani Tupate uzima wa milele. [Tunaitwa] Tuvipofu! Tuvipofu! Tuvipofu! Tuvipofu! 2. Ni kweli Yesu anarudi wenye macho ya kiroho Tayari wameshatambua Wengine tu vipofu hivyo hatuoni lolote. Nyandema SDA Choir. Re 22:12 And, behold, I come quickly; and my reward is with me, to give every man according as his work shall be. Re 22:17 And the Spirit and the bride say, Come. And let him that heareth say, Come. And let him that is athirst come. And whosoever will, let him take the water of life freely.

Itakuwa Siku Moja Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Itakuwa Siku Moja Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Itakuwa siku moja Nitakutanana naye Yesu  Atanifundisha ya kufanya Machoni pake Mungu Refrain Ninajua siku moja Ooh! Nitafurahi daima Nitakaa pamoja na Yesu Uuh! Nikifika mbinguni juu Machozi yangu yatafutwa Ooh! Sitahuzunika tena Taji yangu itang'aa sana Ooh! Nikifika mbinguni juu 2. Kamwe sitamwacha Yesu Japo shetani anitishe Yesu ametangulia mbele Ushindi kwake Mungu Nyandema SDA Choir. Bible Texts Re 7:17 For the Lamb which is in the midst of the throne shall feed them, and shall lead them unto living fountains of waters: and God shall wipe away all tears from their eyes Re 7:16 They shall hunger no more, neither thirst any more; neither shall the sun light on them, nor any heat.

Nyosha Mkono Wako Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Image
Nyosha Mkono Wako Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Kila siku twazidi kuwa wapotovu kwa maadili Mungu alivyoagiza Tunatamani kuwa wakamilifu kama mitume wa zamani Refrain Nyosha mkono wako tufani zavuma Tuma malaika zako tupe nguvu zako Sisi tu wenye dhambi Bwana turehemu Nyosha mkono wako tuweze kushinda (Alleiluia!) 2. Ulinzi wako na uwe pamoja nasi Tupe uwezo wa kushinda majaribu Hatua kwa hatua utupe ushindi Tuongoze katika haki. Nyandema SDA Choir. The "Nyosha mvua la"... Is not very clear and even if it "Nyosha mvua la" it doesn't make sense. This song is also sung by Msanii Music Group. Link; https://youtu.be/ZazkgzbcMyg?si=C_s4bsQYrJGGc_Uf

Waliokombolewa Na Bwana Yesu Lyrics sung by Nyandema SDA Choir

Waliokombolewa Na Bwana Yesu Lyrics sung by Nyandema SDA Choir 1. Waliokombolewa na Bwana Yesu Wataridhi ile inchi ya mbinguni Na tutamwona Yesu mkombozi wetu Akitokea juu mawinguni Refrain Tutapaa mawingu kwa furaha kubwa Tukishikana mikono kwa ushindi wetu Tukiiaga dunia hii yote ya dhambi Kwaheri tuende zetu mbinguni 2. Kwenye bahari ile ya kioo tupu Yesu Mwokozi atatupongeza sana Na tutavikwa taji ya ushindi wetu Oh Allelluia! Asifiwe Mwokozi 3. Vifo magonjwa pia na maombolezo Havitakwepo katika mji ule Wa pekee huo ulioandaliwa  Oh Alleluia! Ndugu usikose. Nyandema SDA Choir. Bible Texts 1Th 4:16 For the Lord himself shall descend from heaven with a shout, with the voice of the archangel, and with the trump of God: and the dead in Christ shall rise first: 1Th 4:17 Then we which are alive and remain shall be caught up together with them in the clouds, to meet the Lord in the air: and so shall we ever be with the Lord. 1Th 4:18 Wherefore comfort one another with these words.

E Mungu Baba Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA

 E Mungu Baba Lyrics sung by Cherubim Singers, Nairobi South SDA 1. E Mungu Baba uliye mbinguni Jina lako Baba litukuzwe (Baba) Ufalme wako Baba na uje Mapenzi yako kwetu yatimizwe 2. Utupe leo riziki yetu Wewe wajua mahitaji yetu (Baba) Utusamehe makosa yetu Tuwasamehe walotukosea 3. Usitutie majaribuni Utuokoe na yule mwovu (Baba) Ufalme nguvu, na utukufu Hata milele zote ni zakat. Outro (Kweli) Msisumbukie ya maisha Baba yenu wa mbingu ajua Bali, tafuta ufalme wa mbinguni Na yote mtazidishiwa Amina. Cherubim Singers, Nairobi South SDA.

We Shall Sing And Praise Him Lyrics sung by The Golden Gate (Chorus)

We Shall Sing And Praise Him Lyrics sung by The Golden Gate (Chorus) Prelude/Refrain We shall sing and praise Him at the Golden Gates Praising God and Jesus all the day and night We shall tell the goodness of the Lord, Our God Come and join us there to sing And praise the Lord. Our God. The Golden Gate Choir. Other oratory parts not added because they are not clear. Attempt to bridge them will be done, God willing.

Tunaye Msaidizi Lyrics sung by The Golden Gate Choir

Tunaye Msaidizi Lyrics sung by The Golden Gate Choir 1. Tunaye msaidizi atupenda Ni mwema kuliko wote atupenda Marafiki duniani hugeuka hutuacha Yeye Yesu hatuachi atupenda, Uuuh 2. Kitu gani anachopenda Bwana Yesu Kutupa baraka zake atupenda Tuvumilie maovu twende kwake Bwana Yesu Tutafika juu mbinguni atupenda, Uuuh 3. Kwa rehema zake Mungu atupenda Tutamushinda Shetani twende mbinguni Leo njoo tujitahidi tutende mapenzi yake Tufike kwake mbinguni atupenda, Uuuh. The Golden Gate Choir.

Yesu Alituahidi/Tunamwona Yesu Akirejea Lyrics sung by The Golden Gate Choir

 Yesu Alituahidi/Tunamwona Yesu Akirejea Lyrics sung by The Golden Gate Choir 1. Yesu alituahidi alipoenda mbinguni Kwamba atarudi tena tuende mbinguni Kwenye makao 'ma yametutayarishia  Ndipo tutaishi milele na mwokozi Chorus Tutamuona Yesu akirejea Kutuchukua kwake kule mbinguni  Ndipo tumuimwimbie kwa shangwe Nyimbo zenye upendo Tukimsifu mwokozi kwa heshima  2. Alitupa roho wa'ke kakae ndani yetu Iliatufundishe mambo ya mbinguni Kwenye maisha mema ambayo ni ya milele Ndipo tutamsifu Yesu Mkombozi 3. Jitahidi ufike mbinguni kwake Mungu Ambao kuna maziwa na asali ya nyuki Hakuna kifo tena wala maumivu Huko ndiko tutamsifu mkombozi, Yesu. The Golden Gate Choir.

The Lord Has Done So Much - Ooh What A Joy Lyrics sung The Golden Gate Choir

The Lord Has Done So Much - Ooh What A Joy Lyrics sung The Golden Gate Choir Oooh..., Aaah..., Uuh... 1. The Lord has done so much for me Now I praise him day and night He has really saved my soul Now, I am free Chorus Ooh - What a joy that will be What a joy that will be What a joy that will be When I see my Lord 2. Jesus Christ is coming soon He is coming for you Are you ready to go with him When he comes 3. Same thing can be done for you If you only trust in him If you invite him in your soul He will come The Golden Gate Choir.

Siku Ambayo Yesu Alikamatwa Lyrics sung The Golden Gate Choir

 Siku Ambayo Yesu Alikamatwa Lyrics sung The Golden Gate Choir 1. Siku ambayo Yesu alikamatwa Makuhani walikutana nyumbani "Wakampotesha uli-kuangika Msalabani kule Gologotha"* Chorus Kwa nini waniacha hapa msalabani Wewe ndiwe Mungu tena Baba yangu Nimekubali kufa niwaokoe Wenye dhambi wote wafike mbinguni 3. Juda Iskarioti msaliti Aliwapa kielelezo kwamba Atamukumumbatia amubusu Ndipo watamtambue Yesu mwokozi 4. Yesu alikamatwa na makuhani Akapigwa sana katemewa mate Akavikwa hata taji ya miba Wakamuangika juu ya musalaba The Golden Gate Choir. "Wakampotesha uli-kuangika Msalabani kule Gologotha"* Not very clear. Could precisely be said as "they organised for his (Jesus) crucifixion on the cross.

Nailed to the Cross Lyrics sung The by Golden Gate Choir

Nailed to the Cross Lyrics sung The by Golden Gate Choir 1. There was One Who was willing to die in my stead, That a soul so unworthy might live; And the path to the cross He was willing to tread, All the sins of my life to forgive.  Refrain They are nailed to the cross! They are nailed to the cross! Oh, how much He was willing to bear! With what anguish and loss Jesus went to the cross, But He carried my sins with Him there. 2. He is tender and loving and patient with me, While He cleanses my heart of the dross; But “there’s no condemnation”—I know I am free, For my sins are all nailed to the cross. 3. I will cling to my Savior and never depart, I will joyfully journey each day, With a song on my lips and a song in my heart, That my sins have been taken away. Written by Carrie E. Breck The Golden Gate Choir.

Mungu Aliwaita Malaika/Huruma Ya Yesu Ya Ajabu sung The by Golden Gate Choir

Mungu Aliwaita Malaika - Huruma Ya Yesu Ya Ajabu sung The by Golden Gate Choir 1. Mungu aliwaita malaika waje kwa mkutano Kaulizwe "nani ataenda kuwaokoa watu?" Refrain Huruma ya Yesu ya ajabu ilimtoa mbinguni Kajitoa afe tuokoke tuwe hai milele 2. Yesu alipotoka juu mbinguni kupigana na dhambi Shetani alidhani atashindwa na kurudi mbinguni 3. Alijaribiwa mara tatu kwa chakula uwezo Kwa kushuka toka juu ya nyumba lakini hakushindwa 4. Jitahidi uwe na imani katika Mungu Baba, Yesu na roho mtakatifu utafika mbinguni. The Golden Gate Choir.

Mikononi Mwa Mungu Lyrics sung The Golden Gate Choir

 Mikononi Mwa Mungu Lyrics sung The Golden Gate Choir 1. Mlango ni wazi kwa wenye dhambi Yesu ndiye anawaita Anahurumia waliokosa Wafikishe kwake ulimwenguni Furaha ni nyingi kwake mwokozi Tutakapofika mbinguni Tutamwimbia nyimbo za shangwe Tumsifu mwokozi - Yesu Chorus Tutapokea taji kwa Yesu - kwake Yesu Mara tutakapofika mbinguni - mbinguni kwake Tutamwimbia nyimbo za shangwe Tumsifu mwokozi - Yesu 2. Ni maji ya bure chota uyanywe Haya maji ni ya uzima Njoo uyapokee uponye kiu Uwe hai kwake milele Furaha ni nyingi kwake mwokozi Tutakapofika mbinguni Tutamwimbia nyimbo za shangwe Tumsifu mwokozi, Yesu 3. Utapumuzika kwake milele Pamoja na Yesu mbinguni - kwetu Utakaribishwa u'pewe zawadi Ndio uzima wa milele Furaha ni nyingi kwake mwokozi Tutakapofika mbinguni Tutamwimbia nyimbo za shangwe Tumsifu mwokozi, Yesu. The Golden Gate Choir.

Njooni Nyote Tumwimbie Lyrics sung The Golden Gate Choir

 Njooni Nyote Tumwimbie Lyrics sung The Golden Gate Choir 1. Njooni nyote tumwimbie tumsifu Yesu Tumwamini mkombozi Yesu mwana Mungu Refrain Ni pendo, Ni pendo la jabu Leo  — Njooni nyote tumwimbie Tulitaje jina lake Ndiye Yesu  — Ni Yesu, Ndiye Yesu  — Ni Yesu, 2. Yesu mkombozi wetu leo yuko nasi Ameleta ukombozi ameshinda dhambi 3. Yesu alishinda mwovu tukapata nguvu Tumaini na Imani Njooni tumwabudu The Golden Gate Choir.

Mikononi mwa Mungu Lyrics sung The Golden Gate Choir

 Mikononi Mwa Mungu Lyrics sung The Golden Gate Choir 1. Mikononi mwa Mungu nimo huketi  Nimo kupumzikia uchovu wote  Mikononi mwa Mungu ni patulivu  Mikononi mwa mungu raha tu Chorus Kote furaha, Amani tele  Furaha kweli, Mikononi mwa Mungu 2. Mikononi mwa Mungu nimo huketi  Nimo hupata maisha yangu ya kweli  Mikononi mwa Mungu hupumzika Mikononi mwa Mungu amani 3. Mikononi mwa Mungu nimo huketi  Nimo hupata amani yangu ya kweli Mikononi mwa Mungu ni raha tupu  Mikononi mwa Mungu amani The Golden Gates, Kampala Uganda.