Posts

Showing posts from September, 2025

Kama Wanaisraeli Lyrics sung by Grace and Glory Singers

Kama Wanaisraeli Lyrics sung by Grace and Grory Singers 1. Kama Wanaisraeli Katika safari yao Safari ya siku chache jangwani Ikawa ya miaka mingi Wengi walikata tamaa Wengi walifia njiani Ni wachache walifika Nchi ya ahadi Ni wachache walifika Nchi ya ahadi Refrain Tutembee kwa ujasiri Kwenye safari ya Kaanani Yesu nahodha wetu ‘tatuvusha salama Bila mwongozo wake Hatuwezi vuka mto Yordani Tujipe moyo tutafika 2. Nasi tunapiga hatua Moja mbele mbili nyuma Katika safari yetu ya mbingu Tupatapo majaribu Tukazeni mioyo yetu sasa Tufikie ng'ambo ya pili Kwani Pwani sio mbali Mwisho tutafika Kwani Pwani sio mbali Mwisho tutafika. Grace and Glory Singers.