Posts

Showing posts from January, 2025

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Tanzania Nakupenda Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania Refrain Tanzania nakupenda nchi yangu nakupenda sana Bara pia visiwani sisi sote tupendane sana 1. Tanzania yetu twakupenda kwa hakika Uumbaji wake Mungu wetu ndio twausifu milele Bahari zake alizotupa ndizo twajivunie leo Bahari zake alizotupa ndizo twajivunie leo 2. Maziwa na vito nazo mbuga za wanyama Mlima mrefu Kilimanjaro upitao yote Afrika Makumbusho yetu ya taifa, ni vivutio kwa wageni Makumbusho yetu ya taifa, ni vivutio kwa wageni 3. Taifa la amani na upendo kwa hao wote Dumisha umoja Mungu Baba, na utuepushe na vita Tupe ulinzi toka kwako Afrika yetu iwe moja Tupe ulinzi toka kwako Afrika yetu iwe moja Acacia Singers, Tz.

Mimi Ni Mungu/Mungu Wa Huruma Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Mimi Ni Mungu/Mungu Wa Huruma Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania 1. Mimi ni Mungu wenu asema Bwana Nirudieni mimi Mungu wa kweli Mnapotanga mbali nasikitika Njooni wanangu sasa rudini nyumbani Refrain Mungu wa huruma tena mwenye na upendo Aita wenye dhambi njooni wanangu 2. Yeye ajaye kwangu sitomtupa Nitampa uzima ule wa milele Kila asikiaye na aje sasa (asema) Nyumbani mwake Baba makao ni mengi 3. Wataoshinda dhambi ‘tavikwa taji Naye Mwokozi Yesu ‘tawakaribisha ‘Ingieni rahani mwa Baba yangu’ Mle mema ya nchi yaloandaliwa Acacia Singers, Tz.

Sikia Neno La Bwana Yesu Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Sikia Neno La Bwana Yesu Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania 1. Sikia neno la Bwana Yesu Alivyosema kwa huzuni, ‘Mikononi mwako Baba yangu. Roho yangu uipokee’ Baada ya hayo Yesu Bwana, Alikataa roho kwa huzuni Baada ya hayo Yesu Bwana, Alikataa roho kwa huzuni Refrain Aliishinda kifo Yesu (wangu) Sasa yu hai Bwana wangu Yauja tena na Malaika Kila jicho litamuona 2. Na ilipokwisha pambazuka Siku ya kwanza ya juma Walikwenda tazama kaburi Tazama lilikuwa tupu Malaika wa Bwana alishuka Akaliondoa lile jiwe Malaika wa Bwana alishuka Akaliondoa lile jiwe  3. Ingawa walilinda kaburi askari wote walishindwa Hofu kuu ilikuja kwao Wakatetemeka kwa uoga Tetemeko kuu la kutisha Wakaanguka kwa nguvu hizo Tetemeko kuu la kutisha Wakaanguka kwa nguvu hizo Acacia Singers, Tz.

Siku Yake Mungu Lyrics sung by Acacia Singers

Siku Yake Mungu Lyrics sung by Acacia Singers 1. Siku yake Mungu inakuja Kwa kila kiumbe juu ya nchi Mungu atamwaga ghadhabu yake kuu Wenye dhambi wote wataangamia Mungu atamwaga ghadhabu yake kuu Wenye dhambi wote wataangamia Refrain Atamwaga ghadhabu yake juu yetu Atawasha hasira yake Atamwaga ghadhabu yake juu yetu Kamwe hatatoa rehema 2. Nani awezaye kusimama Katika hukumu inayokuja Waliokubali kumpokea Yesu Hao ndio watakaokolewa 3. Utasimamaje ukiitwa? Mbele ya kiti cha hukumu ya Mungu Muda umekwisha tumrejee Yesu Siku ile yaja kama vile mwivi Muda umekwisha tumrejee Yesu Siku ile yaja kama vile mwivi. Acacia Singers, Tz.

Nitakufanya Kuta/Acacia Singers Lyrics sung by Acacia Singers

Nitakufanya Kuta/Acacia Singers Lyrics sung by Acacia Singers 1. Nitakufanya kuta wa boma la shaba Hauta bomoshwa milele milele Adui zako wote wapiganapo nawe Hawatakushinda asema Mungu wetu (Hata) Refrain Hata juu mbinguni kwake Tutapokutana naye Acacia Singers wote Tutaimba milele(Hata) 2. Mungu yu na uwezo mkuu ajabu Hatoshindwa kamwe daima milele Tatufanya imara kama mti mshita Acacia kundi ndogo twaimba sifa zake 3. Kama mti mgumo ule wa mshita Uloota wa amani* (kandokando) kando ya kijito Akiwa kati yetu hatutayumbishwa Twaomba Mungu wetu utufanye imara. Acacia Singers, Tz.

Nitakwenda Pekee Yangu Lyrics sung by Acacia Singers

Nitakwenda Pekee Yangu Lyrics sung by Acacia Singers 1. Nitakwenda kwake mimi pekee yangu Nasikia aniita “Njoo kwangu Wewe utaabikaye Pekee yako itakoma,” Asema Bwana “Mimi ndiye chakula ya uzima Yeye alaye hataona njaa Yeye alaye hataona njaa Refrain Yesu asema, "Njooni nyote kwangu Furaha amani mtapata mbinguni." 2. Niambie u tayari kumwandama Uende naye mbinguni Je una shaka na hutaki kumwamini? Au bado watamani raha za dunia? Hatujui yatakayo jiri kesho Mfuata Yesu upate uzima Mfuata Yesu upate uzima 3. Wateule watakwenda naye Bwana Kuishi huko mbinguni Kwa furaha wamwimbie nyimbo tamu  Za utukufu kwa shangwe wakiwa juu Utukufu wake Mungu utang’aa Walotakaswa wataishi humo. Acacia Singers, Tz.

Ondoka Uangaze Lyrics sung by Acacia Singers

Ondoka Uangaze Lyrics sung by Acacia Singers 1. Ondoka uangaze kwa kuwa nuru ya Bwana imekuja Na utukufu wa Bwana umekuzukia  Ondoka peleke neno utangaze kwa wote  Refrain Wajulishe habari kwamba yu mlangoni Anarejea upesi Mwokozi Wajulishe wote kwamba yuko karibu 2. Amka harakishe usisubiri kwani muda waisha Mavuno ni tayari wavuni wachache Ondoka peleke neno utangaze kwa wote. Acacia Singers, Tz.

Ungeniambia Nilipokosea Lyrics sung by Acacia Singers

Ungeniambia Nilipokosea Lyrics sung by Acacia Singers 1. Ungeniambia nilipokosea Nikalijua kosa langu Uenda ningebadilika Nikajirekebisha Umeifanya dhambi yangu Kunuka mbele za watu Mdahalo wote juu yangu Kwa kosa nisilojua Iiii Iiii Maneno haya yanahuruma Ungeniambia nilipokosea Nami nikabadilika 2. Maneno yanayonenwa juu yangu Yanaumiza roho yangu Laiti kama ungenijulisha Nikajua ubaya wangu Ungeniita kwa upole Ukanieleza kwa pendo Ungeiokoa nafsi yangu Kwa haya yatokeayo  3. Leo* uamue uje kwa Yesu Aliye msaada wetu Hakika Bwana wetu atupenda Yeye ana huruma nyingi Hutuonya kwa upole, "Msitende dhambi wanangu," Yeye husamehe, husahau Wala hakumbuki tena Outro Yesu utusaidie tuvishe *Tufike mbele sote Tufike mbinguni. Acacia Singers, Tz.

Ninakushukuru Kwa Wema Wako Lyrics sung by Acacia Singers

Ninakushukuru Kwa Wema Wako Lyrics sung by Acacia Singers 1. Ninakushukuru kwa wema wako Mungu mtukufu wa kuabudiwa Wewe ndiwe mponya na hakuna mwingine Umenishindia yaliyo makuu Wewe ndiwe mponya na hakuna mwingine Umenishindia yaliyo makuu Refrain Ni wewe tu Bwana Mungu wangu Wala hakuna yeyote kama wewe Ni wewe tu Bwana Mungu wangu Ndiwe mfariji wangu hakuna mwingine 2. Uweza na nguvu (Yote) na mamlaka Yashinda wakuu wote wa dunia Nionapo milima, jua, mwezi na nyota Wewe ni mkuu haulinganishwi Nionapo milima, jua, mwezi na nyota Wewe ni mkuu haulinganishwi 3. Nikifika kwako huko mbinguni Nitakusujudu we mtakatifu Sifa na heshima viwe nawe milele Watu maelufu kukusujudia Sifa na heshima viwe nawe milele Watu maelufu kukusujudia. Acacia Singers, Tz.

Ninakushukuru Kwa Wema Wako Lyrics sung by Acacia Singers

Ninakushukuru Kwa Wema Wako Lyrics sung by Acacia Singers 1. Ninakushukuru kwa wema wako Mungu mtukufu wa kuabudiwa Wewe ndiwe mponya na hakuna mwingine Umenishindia yaliyo makuu Wewe ndiwe mponya na hakuna mwingine Umenishindia yaliyo makuu Refrain Ni wewe tu Bwana Mungu wangu Wala hakuna yeyote kama wewe Ni wewe tu Bwana Mungu wangu Ndiwe mfariji wangu hakuna mwingine 2. Uweza na nguvu (Yote) na mamlaka Yashinda wakuu wote wa dunia Nionapo milima, jua, mwezi na nyota Wewe ni mkuu haulinganishwi Nionapo milima, jua, mwezi na nyota Wewe ni mkuu haulinganishwi 3. Nikifika kwako huko mbinguni Nitakusujudu we mtakatifu Sifa na heshima viwe nawe milele Watu maelufu kukusujudia Sifa na heshima viwe nawe milele Watu maelufu kukusujudia. Acacia Singers, Tz.

Nguvu Zangu Pekee Lyrics sung by Acacia Singers

Nguvu Zangu Pekee Lyrics sung by Acacia Singers 1. Nguvu zangu pekee hazitoweza Kupambana naye Ibilisi Jeshi lake kubwa huniandama Kote niendako hunitisha Refrain Nakuita mchungaji mwema (Yesu) Yesu mwana wa Mungu (Kweli) Nipitapo kati ya nyika Bwana nisiogope 2. Ewe Mungu wangu nisaidie Ona nasumbuka na mateso Mzigo mzito niliobeba Tautua kwako nipumzike 3. Masumbuko haya mpaka lini? Bwana wangu Yesu niahidi Tutapokutana makao mapya Baba mama wote niwaone Refrain Nakuita mchungaji mwema (Yesu) Yesu mwana wa Mungu (Kweli) Nipitapo kati ya nyika Bwana nisiogope 4. Ninapotazama juu mbinguni Naiona nyota ile tukufu Tukufu kwa wale wasafirio Kwa machozi mengi Bwana Yesu Refrain Nakuita mchungaji mwema (Yesu) Yesu mwana wa Mungu (Kweli) Nipitapo kati ya nyika Bwana nisiogope. Acacia Singers, Tz.

Sisi Tu Wasafiri Lyrics sung by Acacia Singers

Sisi Tu Wasafiri Lyrics sung by Acacia Singers 1. Sisi tu wasafiri wa kwenda mbinguni Dunia si kwetu, kwetu ni mbinguni Muda u mbele yetu umeamuliwa juu Na dunia hii kukomesha dhambi 2. Maisha ya dunia yamejaa mashaka Mambo ya dunia yote yanapita Yapaswa tujihoji tumeanguka wapi Tumrudie Yesu yeye ndiye njia. Acacia Singers, Tz.

Sina Hofu Wala Mashaka Lyrics sung by Acacia Singers

Sina Hofu Wala Mashaka Lyrics sung by Acacia Singers 1. Sina hofu wala mashaka Kwani Yesu yu ndani yangu Aongoza hatua zangu Popote nitembeapo Refrain Nakaza mwendo Nasonga mbele Japo njia ni ndefu Dhiki taabu Nayo mateso Kwa imani mimi nitafika  2. Japo njia ina mabonde Yote hayo mi' sitahofu Ninajua niko salama Mwendo nitaumaliza. Acacia Singers, Tz.

Naamani Shujaa Wa Jeshi Lyrics sung by Acacia Singers

Naamani Shujaa Wa Jeshi Lyrics sung by Acacia Singers 1. Shujaa wa jeshi lile la washami Mtu mkubwa jemedari mkuu wa vita Muheshimiwa alishinda vita nyingi Ni Naamani lakini alikuwa mkoma Refrain Mara saba ukaoge Yorodani Utakaswe ngozi yako utapona  2. Binti yule mfungwa mfanyakazi Mu-Isiraeli aliyejawa huruma Alitamka laiti angekuwepo Nabii yule wa Msamaria angepona 3. Sasa tazama najua yote hakika Hakuna Mungu humu duniani mwote Ila katika Israeli pekee Alitamka Naamani alipoponywa Outro 1 Huyu Mungu muumbaji Ndiye Mungu Bwana wetu Anayeponya magonjwa Na kutenda maajabu  Outro 2 Njoo utakaswe dhambi zako Usafishwe naye (na Yesu) kwa damu yake. Acacia Singers, Tz.

Punda Mwana Punda Lyrics sung by Acacia Singers

Punda Mwana Punda Lyrics sung by Acacia Singers Chorus Endendeni katika kile kijiji kile kinachowakabili (Ndipo) Mtamwona punda kafungwa na mwanapunda Pamoja naye wafungueni nanyi mnilete Mkiulizwa semeni Bwana anawahitaji Mkiulizwa semeni Bwana anawahitaji 1. Wakaenda zao wale wanafunzi Wakafanya vile alivyowaamuru Shangwe furaha tele mji wote Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwana Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwana (Sasa) 2. Sababu ya furaha walokuwa nayo Walitandika nguo zao njia yote Wakiwa na matawi mikononi Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwan Waliimba Hosana ajaye kwa jina la Bwana (Sasa) 3. Njooni tumwimbie Yesu Bwana wetu Kwa ushindi mkuu natumtukuze Njooni tumsifu mkombozi Huyu ndiye Yesu Mwokozi wa maisha yetu (Haleluya) Huyu ndiye Yesu Mwokozi wa maisha yetu. Acacia Singers, Tz.

Mtafuteni Bwana/Wajane Lyrics sung by Acacia Singers

Mtafuteni Bwana/Wajane Lyrics sung by Acacia Singers Uuuh, Uuuh, Uuuh 1. Mtafuteni Bwana kwani anapatikana Mwombeni wakati wote yeye yu karibu Hujibu maombi kwa wote wamwitao Ikiwa usiku mchana hata asubuhi Ikiwa usiku mchana hata asubuhi Refrain Ooh Baba (Baba), Ooh Mungu wangu Uwasikie wote waliao Nawe uwape usingizi Ooh Yesu (Yesu), Ooh Mungu wetu Wajane wote uwape amani Uwarehemu na yatima  Aaah, Aaah, Aaah, Aaah 2. Ni ahadi yake yeye aliyoitoa Yeyote ajaye kwangu sitamtupa kamwe Na wimbi la shida lijapokuandama Muite Bwana Yesu useme naye kwa upole Muite Bwana Yesu useme naye kwa upole Acacia Singers, Tz.

When the Rich and the Poor Get Together Lyrics sung by The Gospel Train

When the Rich and the Poor Get Together Lyrics sung by The Gospel Train (When We All Get Together With The Lord Lyrics) (Now) When the rich and the poor get together with the Lord Get together, get together with the Lord They will treat each other like sister and brother When they all get together with the Lord Refrain (Now) When we all get together (Hallelujah) When they all get together with the Lord They will treat each other like sister and brother When they all get together with the Lord (Now) When the tall and the short get together with the Lord Get together, get together with the Lord They will treat each other like sister and brother When they all get together with the Lord (Now) When the big and the small get together with the Lord Get together, get together with the Lord They will treat each other like sister and brother When they all get together with the Lord The Gospel Train. This version has a wording variation to the one done by The Gaither's Band.

Twaja Mbele Zako Lyrics sung by Acacia Singers

Twaja Mbele Zako Lyrics sung by Acacia Singers 1. Twaja mbele zako, Tu wanyonge kabisa Twaleta dhambi zetu, Ili utukomboe Tunakuja jinsi tulivyo, Utuoshe kwa damu yako Refrain Pekee yangu sitaweza  Kuvumilia mateso  Njoo Yesu mkombozi wangu 2. Pekee sitaweza, Kuumshinda Shetani Kama utaniacha, Sitaweza Mkombozi U mlinzi na ngome yangu, Msaada ulokaribu. Acacia Singers, Tz. Ps 55:22 Cast thy burden upon the LORD, and he shall sustain thee: he shall never suffer the righteous to be moved. Matthew 11:29-30 Take my yoke upon you, and learn of me; for I am meek and lowly in heart: and ye shall find rest unto your souls. For my yoke is easy, and my burden is light. Psalms 68:19-20 Blessed be the Lord, who daily loadeth us with benefits, even the God of our salvation. Selah. He that is our God is the God of salvation; and unto GOD the Lord belong the issues from death. 1 Peter 5:6-7 Humble yourselves therefore under the mighty hand of God, that he may exalt you in due time: Casting a...

Makaoni Mwake Lyrics sung by Acacia Singers

Makaoni Mwake Lyrics sung by Acacia Singers 1. Makaoni mwake Bwana nitaketi Nile naye, nizungumze naye Furahani mwake Bwana nitaketi Nimwimbie wimbo mutamu Nikiwa na amani na furaha moyoni mwangu Nikiwa na amani na furaha moyoni mwangu Refrain Furaha yangu nifike juu Yesu Mwokozi anipokee Nitaimba na Malaika Nyimbo nzuri nikimsifu Bwana 2. Mji wake Mungu niutamanio Kuna raha isiyo kifani, aah Wote walochoka watapumzishwa Yesu Kristo atawafariji (kweli) Kwenye mji wa Mungu ‘taishi naye Bwana wangu Kwenye mji wa Mungu ‘taishi naye Bwana wangu 3. Tutakusanyika toka kila pembe Kulitukuza jina la Yesu Malango ya lulu yatafunguliwa Naye Yesu Mkombozi wetu Sikia nikueleze kuna raha kule kwa Baba Sikia nikueleze kuna raha kule kwa Baba Acacia Singers, Tz.

Huyu Yesu Mnazorayo Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania

Huyu Yesu Mnazorayo Lyrics Sung by Acacia Singers, Tanzania Verse 1 Huyu Yesu, ataitwa mnazorayo Huyu Yesu, ataitwa mnazorayo Twakueleza habari zake Yesu Aliyeishi kama maskini Akalelewa Yesu mjini Nazareti Wakaazi wa mji huo Wakamwita mnazorayo Ata akakuwa akihubiri kote Neno la uzima katika miji yote Ata akakuwa akihubiri kote Neno la uzima katika miji yote Aliitwa mnazorayo Aliitwa mnazorayo Verse 2 Alikamatwa Yesu mnazorayo Akapelekwa mbele ya makuhani Akaeleza Yesu, “Nalikuwa nanyi, Siku zote hekaluni nikiwafundisha nyote Lipi nililotenda kwenu watu wangu lililobaya kwenu nanyi mwanikamata? Lipi nililotenda kwenu watu wangu lililobaya kwenu nanyi mwanikamata?” Break Aaa-uuh, Aaah-Aaah Aaa-aah, Aaah-Uuuh-Aliteswa! Verse 3 Aliteswa Yesu mnazorayo Aliteswa Yesu mnazorayo Akaangikwa pale juu Goligotha Yesu kalia Eloi, Eloi, Lama Sabakthani?" Yaani "Mungu wangu, Mbona sasa waniacha," Alilia Yesu masikini Taji ya miba kawekewa kichwani Wale Wayahudi hawakumfahamu Taji ya ...

Miaka Yangu Ni Michache/Neema Yako Lyrics sung by Acacia Singers

Miaka Yangu Ni Michache/Neema Yako Lyrics sung by Acacia Singers 1. Miaka yangu ni michache Maisha yangu yamejaaa taabu Sijaona furaha maishani mwangu Yakiwa mafupi kamwe sitahuzunika Refrain Neema yako Eeh Bwana Ndiyo twaitumaini Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha 2. Mara nyingi shetani hunisongaa Hunionyesha shida, njaa, vita, Magonjwa na mauti watu wakisumbuka Kusudi nimwache Yesu Mkombozi wangu Acacia Singers, Tz. Ps 90:10 The days of our years are threescore years and ten; and if by reason of strength they be fourscore years, yet is their strength labour and sorrow; for it is soon cut off, and we fly away Psalm 39:4-6 “Lord, make me to know my end And what is the extent of my days; Let me know how transient I am. “Behold, You have made my days as handbreadths, And my lifetime as nothing in Your sight; Surely every man at his best is a mere breath. Selah. “Surely every man walks about as a phantom; Surely they make an uproar for nothing; He amasses riches and does not know who ...

Yesu Uje Kwangu Lyrics sung by Acacia Singers

Yesu Uje Kwangu Lyrics sung by Acacia Singers 1. Yesu uje kwangu, Ukae kwangu moyoni Unipe badiliko la pekee, unifanye niwe nuru kote Nauamini uwezo wako, Yesu haushindwi jambo lolote Refrain Yote yawezekana Kwa jina lake Yesu Kila anayemwendea Yesu atampokea 2. Bwana nakumbuka,  Huruma zako za ajabu Ulimsamehe Mariamu, Aliposhitakiwa kwako Hivyo ulitenda kwa Rahabu, Alipokufuata kwa imani 3. Damu yake Yesu, Husafisha makosa yetu Aliangikwa msalabani,  Akawa kafara ya aibu  Hebu sikieni wito huu,  Njooni tumsifu Mwokozi wetu. Acacia Singers, Tz. Ps 51:10 Create in me a clean heart, O God; and renew a right spirit within me. Zaburi 51:10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. 1Jo 1:9 If we confess our sins, he is faithful and just to forgive us our sins, and to cleanse us from all unrighteousness. 1Yohana 1:9 Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote. ...

Tawala Ndani Yangu Lyrics sung by Acacia Singers

Tawala Ndani Yangu Lyrics sung by Acacia Singers Verse 1 Tawala ndani yangu Muumbaji Mfalme Unilinde na dhoruba zinazonizunguka Kama mawimbi ya bahari yavumayo kwa nguvu Ndivyo shetani na jeshi lake anavyonitafuta Ndivyo shetani na jeshi lake anavyonitafuta Verse 2 Ukae ndani yangu wakati ni mfupi Popote nitembeapo uniongoze Yesu Ata mwisho wa safari hii nikuone karibu Uliyetoa uhai wako kwa wote wenye dhambi Uliyetoa uhai wako kwa wote wenye dhambi Verse 3 Tazameni ramani bandari ii karibu Wala usichoke ndugu Mwokozi angojea Tutapofika Yerusalemu tutamuona Yesu Ndipo atafuta kila chozi huzuni zitakwisha Ndipo atafuta kila chozi huzuni zitakwisha Outro Utawale ndani yangu, utawale, tawala ndani Utawale ndani yangu, utawale, Bwana wangu tawala(*4) Acacia Singers, Tz.

Habari Za Kuzaliwa Lyrics sung by Acacia Singers

Habari Za Kuzaliwa Lyrics sung by Acacia Singers 1. Habari za kuzaliwa kwake Bwana Yesu Zilienea mjini Bethlehemu [Ma-] Majusi toka mashariki walifika Kuja kumuona Mwokozi wa dunia hii Refrain Waliiona nyota ya mashariki (ndipo) Wakaondoka wote kwa furaha kuu Walipofika kule Bethlehemu Walimsujudia Yesu (wote) 2. Uwezo toka kwake Roho mtakatifu Alizaliwa katika hori la ng'ombe Imanueli yaani Mungu yu pamoja nasi Tuziimbe sifa Mwokozi amezaliwa 3. Na Herode alipoupata ujumbe  Kazaliwa mfalume wa Uyahudi Alighadhabika ndipo kaua watoto Wa kiume wote katika mji ule. Acacia Singers, Tz. Lu 1:14 And thou shalt have joy and gladness; and many shall rejoice at his birth. 1 Samuel 1:27–28 NIV "I prayed for this child, and the LORD has granted me what I asked of him. So now I give him to the LORD. For his whole life he will be given over to the LORD." Psalm 8:1-2 NIV Lord, our Lord, how majestic is your name in all the earth! You have set your glory in the heavens. Through the pra...

Bwana Utakaporudi Lyrics sung by Acacia Singers

Bwana Utakaporudi Lyrics sung by Acacia Singers 1. Bwana utakaporudi Kama jinsi ulivyoahidi Shida taabu za dunia hii Zitakoma nikiwa nawe Refrain Ombi langu ujapo unikumbuke Katika uzima wa milele Utapoita wateule wako Jina langu unikumbuke 2. Nilitanga mbali nawe (na) Tena nilipotea gizani Kama kondoo nilipotea Ukanirejesha zizini 3. E mwamba na ngome yangu Unisikie ninapokwita Niokoe katika hatari Na mateso yake Shetani. Acacia Singers, Tz. Psalms 25:7 “Remember not the sins of my youth, nor my transgressions: according to thy mercy remember thou me for thy goodness' sake, O LORD.” Luke 23:42 And he said unto Jesus, Lord, remember me when thou comest into thy kingdom. Psalm 136:23 He remembered us in our weakness. His faithful love endures forever.

Tutangaze Habari Lyrics sung by The Gospel Train

Tutangaze Habari Lyrics sung by The Gospel Train 1. Tutangaze habari zake Bwana Tuendeni muda umekwisha (waisha) Wapo wengi waliolala humu Tuendeni tumtangaze Bwana Refrain Nuru yake Bwana iangaze Waliopotea tuwatafute Tutangazeni neno hili la Bwana Muda kitambo Bwana a'rejea 2. Neno hili la ufalme wa Mungu Tulieneze duniani kote Mtu asijelia hakujua Tuendeni tumtangaze Bwana  Outro Dada twende, twende Twende tuhubiri neno lake Bwana Mwokozi Tusambaze kote twende tuhubiri Ndugu twende, twende Twende tuhubiri neno lake Bwana Mwokozi Tusambaze kote twende tuhubiri Ewe twende, twende Twende tuhubiri neno lake Bwana Mwokozi Tusambaze kote twende tuhubiri Kijana twende, twende Twende tuhubiri neno lake Bwana Mwokozi Tusambaze kote twende tuhubiri Dada twende, twende Twende tuhubiri neno lake Bwana Mwokozi Tusambaze kote twende tuhubiri Dada twende... The Gospel Train, Kenya.

Japokuwa Safari ni Ndefu Lyrics sung by The Gospel Train

Japokuwa Safari ni Ndefu Lyrics sung by The Gospel Train 1.Japokuwa safari ni ndefu Pande zote dhoruba mawimbi Nina ujasiri Yesu yuko mbele Mimi siogopi namwamini Yesu Refrain 1 Shetani aniwinde ili animalize Mimi simwogopi namwamini Yesu Anifanye mgonjwa ili animalize Mimi siogopi namwamini Yesu Safarini anitege ili animalize Ajali siogopi namwamini Yesu Usiku akitisha ninaye mkombozi Mungu mwenye upendo nimemwamini Yesu 2. Kwa hakika ndugu una mengi Moyo wako unao uzito Kuna jina moja ukiliita leo U’tapata pumziko jina hilo ni Yesu Refrain 2 Shetani atakuwinda ili akumalize Mimi nakushauri ita jina la Yesu Akufanye mgonjwa ili akumalize Bado nakushauri ita jina la Yesu Akikutega njiani ili akumalize Tena nakushauri ita jina la Yesu Usiku akitisha unae mkombozi Mungu mwenye upendo ita jina lake Outro Na sisi hatutishwi Tunaye mkombozi Mungu mwenye upendo Tumemwamini Yesu The Gospel Train.

Namkaribisha Yesu Lyrics Sung by The Gospel Train

Namkaribisha Yesu Lyrics Sung by The Gospel Train Refrain Namkaribisha Yesu atawale ndani yangu Dunia imechafuka, shida nyingi na majonzi Najitoa kwake atawale ndani yangu Hivyo ataniwezesha kuihama dunia hii 1. Nilikuwa mdogo sana kule tumboni mwa mama Lakini akanilinda mpaka nilivyozaliwa Wakati nikiwa mdogo akanilinda kanitunza Maisha yake nimeipata namkaribisha Yesu (Huyu Yesu) 2. Nilikuwa mwovu sana mdanganyifu mwenye dhambi Lakini kwa uwezo wake akanigeuza niwe mwema Nikasikia sauti yake Yesu nikaitika Nikapata utakatifu nimekaribisha Yesu (Huyu Yesu) The Gospel Train, Kenya.

Hebu Tumheshimu Bwana Lyrics sung by The Gospel Train

Hebu Tumheshimu Bwana Lyrics sung by The Gospel Train 1. Hebu tumheshimu Bwana muumba wa vitu vyote Uwezo wake ni mkuu kwa watu wake, eeeh Tangu utotoni mwetu ametulinda muumba Nitamshukuru, nitamshukuru Mungu wangu Refrain Anastahili heshima Mungu wetu Yeye ni Mungu, ni Mungu wa Baba zetu Tunapaswa kutangaza Mungu wetu Hatuwezi kunyamaza, Mungu ni mkuu 2. Najua mimi mnyonge, mwili wangu ni dhaifu Bila Mungu sina nguvu wala uwezo (wala uwezo) Ninajitoa mhanga kwake aliye muweza Naegemea kwake mwenyezi Mungu wangu. The Gospel Train, Kenya.

Bwana Wangu Yesu Aliteseka Lyrics sung by The Gospel Train

Bwana Wangu Yesu Aliteseka Lyrics sung by The Gospel Train 1. Bwana wangu Yesu aliteseka Msalabani kwa ajili yangu Ili anikomboe kwa dhambi zangu Moyo wangu unaburudika (Kweli) Refrain Nina furaha moyoni mwangu Nitakusifu maishani yangu yote (ewe Bwana) Ulikomboa kwa damu yako Ili niwe mwana wako kamili (Baba) 2. Mungu wa Ibrahimu,Mungu wa Isaka Nakumbuka maajabu uliyotenda Katika maisha yangu miujiza uliyotenda Inadhihirisha ukuu wako kwangu (Bwana) 3. Sasa imebakia kuona uso wako Kwa kuja kwako mara ya pili Unitayarishe kwa siku hiyo Ili niwe kati ya wa'o waendao (Bwana). The Gospel Train, Kenya.

Zamani Nilikuwa Lyrics sung by The Gospel Train

Zamani Nilikuwa Lyrics sung by The Gospel Train 1. Zamani nilikuwa mdhambi mpotevu Nilizama dhambini bila matumaini Nilikuwa katikati ya misitu mwenzangu Shetani alinitega na mitego yake Refrain Asante Yesu kwa pendo lako Ulonionyesha pale msalabani Ulinitafuta mimi mdhambi Kwa kifo chako Bwana nimekuwa huru 2. Mara ngapi umejikuta katika shimo la dhambi Je wakumbuka pendo lake Yesu Bwana wa upendo Alitufia kasulubiwa sote tupate wokovu Nitaimba pendo lake na nitamuinua The Gospel Train.

One Day Jesus Will Call My Name Lyrics sung by The Gospel Train

One Day Jesus Will Call My Name Lyrics sung by The Gospel Train Refrain One day Jesus will call my name As days go by, Hope I don’t stay the same I wanna get so close to Him there's no big change On that day that Jesus calls my name 1. Some days drag and Some days fly Some days I think of the day I’ll die Some days fill me and some days drain But one day Jesus will call my name 2. Now most days I pray but some days I curse A number of days I put myself first But it’s not what I do, the cross made that plain And one day Jesus will call my name. The Gospel Train. This song also sung by Lynda Randle. This version is slightly different in wording from the original from lyrics.